Waziri wa Michezo azindua mbio za marathoni Olympic Fit kama uungaji mkono kwa kongamano la kilele la tabianchi kwa ushiriki wa wanariadha 300 kutoka nchi 30


Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, Alhamisi kupitia video conference, alizindua dalili ya kuanza mbio za marathoni (El Fit) katika hifadhi ya (Wadi Degla) kama moja ya matukio ya Olympic Fit kuliunga mkono kongamano la kilele cha tabianchi mjini Sharm Elsheikh na wanariadha 300 kutoka nchi 30 walishiriki marathoni hiyo.


Mpango wa Olympic Fit unafanyika miongoni mwa mpango wa Rais wa Jamhuri Abdel Fatah El Sisi (Michezo ni mtindo wa maisha), kwa uangalizi wa Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo na kwa uratibu wa Muungano wa kimisri wa michezo ya mtaa na siha ya ushindani kwa ushirikiano na Shirikisho la kimataifa la siha ya ushindani.


Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alisema:"Mashindano ya Olympic Fit ni maendeleo ya mpango wa Wizara wa uandaaji na uenyeji wa matukio ya kimchezo ya kimataifa nchini Misri unaolenga kuimarisha utalii wa kimchezo na kuwatia moyo vijana kuzoea michezo na kutunza afya zao kwa ujumla ili kujenga miili ya kiafya".


Waziri akaongeza kuwa Shirikisho la kimisri la michezo ya mtaa na siha limefanikiwa mnamo muda mfupi kuwavutia vijana wamisri wengi kuzoea michezo kwa kupitia michuano inayotekelezeka nalo iwe katika ngazi ya kitaifa au ya kimataifa.


Ilhali Islam Qurtam, Mkuu wa Shirikisho la kimisri la michezo ya mtaa na siha, alieleza kuwa Shirikisho linachapa kazi kukufanya kuzoea michezo kuwe tabia ya kila siku maishani mwa wavulana na wasichana nchini Misri, na hivyo kujenga miili mizima ya kiafya, akionesha kuwa Waziri wa Vijana na Michezo ni muungaji mkono wa kwanza wa Shirikisho hilo.


Akaendelea kuwa mbio za marathoni zinaimarisha kongamano la kilele cha tabianchi lifanyikalo mjini Sharm El Sheikh، akionesha kwamba Vijana wamisri wanahitaji misaada kutoa juhudi zake zote kwa usahihi, hivyo mfano wa michezo midogo kama hii inawasaidia na kuwaelekeza njia iliyo sahihi.


Matukio ya Olympic Fit, yanayoendelea kwa miezi mitatu, yanajumuisha michuano ya (Jamhuri kwa siha ya ushindani) inayofikisha  michuano ya ulimwengu nchini Mexico mtandaoni, kwa ushiriki wa wachezaji 500 (wavulana na wasichana) pamoja na uandaaji wa michuano 8 mbalimbali katika klabu (El Nadi) katika "Mji mkuu wa Utawala" mnamo  10 hadi 12 Novemba hii kwa ushiriki wa wachezaji wamisri na wageni 4000 (wavulana na wasichana) wanawakilisha nchi 40, huo ni mchuano wa (El Fit kwa siha ya ushindani) na unajumuisha mashindano kama vile: (mbio, kuogelea, kunyanyua uzani, siha ya ushindani), unaofikisha mchuano wa (cross fit) wa kimataifa, mchuano wa Calisthenics, mashindano ya Strong man, mashindano ya Rowing, mashindano ya michezo mitatu ya kiushindani (mbio, kuogelea, baiskeli), mashindano ya Juniors kwa siha ya ushindani, mashindano ya Lift It, mashindano ya Rookies, pamoja na kushiriki katika matukio ya mbio za marathoni za Zayed na uratibu wa michuano ya vyuo vikuu na ligi ya shule Januari ijayo.

Comments