Wizara ya michezo yahitimu toleo la 17 la kongamano la Vijana la mkataba wa mfumo wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi COY17
- 2022-11-18 19:14:33
Wizara ya Vijana na Michezo ilizihitimu shughuli za toleo la 17 la kongamano la Vijana la mkataba wa mfumo wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi COP27, ambalo limefanyika mjini mwa vijana, Sharm El Sheikh mnamo (2-4) Novemba hii kwa usimamizi wa idara rasmi ya mzunguko wa vijana ya mkataba wa mfumo wa Umoja wa Mataifa juu ya mabadiliko ya tabianchi, pia, kwa uungaji mkono wa Umoja wa Mataifa nchini Misri na idadi ya ofisi zake kama ofisi ya UNICEF, Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa idadi ya watu, programu ya kimaendeleo ya Umoja wa Mataifa, Shirika la afya Duniani, ofisi ya UNESCO, pamoja na Shirika la kimataifa la uhamiaji, ofisi ya wanaojitolea wa Umoja wa Mataifa, ofisi ya makubaliano ya kimataifa ya Umoja wa Mataifa kwa ushiriki wa kimisri na kwa ushiriki wa mashirika 5 ya kivijana ya kimisri nayo ni (Acts, Envirox, El Emam, vijana wanaipenda Misri, you thing green).
Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, Bw. Simon Steel, katibu mtendaji wa mkataba wa mfumo wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi (UNFCCC), Balozi Wael Abu El Magd, mwakilishi binafsi wa mwenyekiti wa kikao cha 27 cha mkutano wa nchi wanachama wa mkataba wa mfumo wa Umoja wa Mataifa juu ya mabadiliko ya tabianchi "COP27", Bw. Francisco Rota, kiongozi wa shirkisho la kimataifa la vyama vya msalaba mwekundu na hilali nyekundu, Bi. Frederica Mayer, mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu nchini Misri, Bw. Germy Hopkins, mwakilishi wa UNICEF nchini Misri, Balozi Amr Essam, mwakilishi wa Wizara ya mambo ya nje, Dkt. Omnia El Omrany, mjumbe wa mwenyekiti wa kongamano la vijana COP27, Meja Jenerali Ismael El Far, kiongozi wa sekta ya vijana kwenye Wizara ya Vijana na Michezo na viongozi wa Wizara ya Vijana na Michezo walihudhuria sherehe ya kuhitimu.
Wakati wa hotuba yake, Waziri wa Vijana na Michezo, alisema :"leo, tunafurahi kufikia nyakati hizi za furaha zinazopongeza juhudi zote za watu kwa ushindi wa uenyeji wa Misri wa toleo la 17 la kongamano la vijana la mabadiliko ya tabianchi COY17 kwa ushirikiano wa juhudi zote za Misri zilizowakilishwa na taasisi ramsi na mashirika ya vijana, isitoshe, uungaji mkono wa uongozi wa kisiasa kwa juhudi hizo kuhifadhi mazingira kutokana na kukumbwa na mabadiliko ya tabianchi, hivyo serikali ya kimisri inakuja mbele kwenye matukio ya kimataifa kwa ufadhili wa uongozi wa kisiasa."
Sobhy akaongeza:"leo, tulifikia lengo kuu la kongamano hilo ambalo ni kuzingatia maoni ya vijana kwenye mchakato wa uamuzi na kuweka sera za kimataifa zinazohusiana na tabianchi, haswa kwa kuwa suala la mabadiliko ya tabianchi lina umuhimu zaidi ulimwenguni", akithamini juhudi zilizofanywa na walioshiriki kutoka nchi mbalimbali katika kuandika mapendekezo ya kongamano kwa jina la vijana wa Dunia.
Waziri wa Vijana aliyashukuru mashirika na taasisi zilizoshiriki uandaaji kwa juhudi zake zote katika uenyeji wa kongamano la Vijana la mabadiliko ya tabianchi mjini Sharm El Sheikh, akionesha kuwa Wizara ya Vijana na Michezo ya kimisri inajaribu kuwaunganisha vijana kupitia mipango ya COP17 katika mfumo wa siku maalum "vijana na vizazi wajao" itakayofanyika Novemba 10.
Sherehe hiyo ilishuhudia kukabidhi hati ya vijana ya sera za kimataifa zinazohusu vijana na ambazo zilijumuishwa na nchi zote Duniani ili vijana waweze kuwakilisha sauti za vijana kwenye kongamano la COP27.
Kongamano la Vijana la mkataba wa mfumo wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi COY17 linazingatiwa tukio kubwa na muhimu zaidi la vijana linalochangia kujenga uwezo na kuzoea sera kuwaandaa vijana kushiriki kongamano lijalo la tabianchi, ambapo linajumuisha maelfu ya wanaofanya mabadiliko kutoka kwa zaidi ya nchi 140, vilevile linachukuliwa kama mkusanyiko muhimu zaidi wa vijana, likiweza kuwaelekeza msimamo rasmi wa vijana moja kwa moja kwenye mazungumzo ya Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi, miongoni mwa hati muhimu zilizotolewana COY17 ni pamoja na hati ya sera ya kimataifa iliyoamuliwa maandiko yake kutokana na sauti za vijana ulimwenguni kote na ambayo itaangaliwa kwa kina wakati wa mazungumzo ya Umoja wa Mataifa kuhusu tabianchi.
Comments