Waziri wa Michezo ashughulikia Ushirikiano na Mwakilishi wa Umoja wa Afrika kwa Afya,Masuala ya kibinadamu na Maendeleo jamii



Dkt.Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo alikutana na Balozi Menata Samati Sisuma, Mwakilishi wa Umoja wa Afrika kwa Afya, Masuala ya kibinadamu na Maendeleo jamii ili  kujadiliana kuhusu njia za Ushirikiano wa pamoja, kwa mahudhurio ya Rwandi Sugilar,Mkurugenzi wa Ofisi ya kiutendaji wa kupambana na dawa za vichocheo kwa ngazi zote Barani  Afrika (AL RADO),na Dkt.Hazim Hamis, Mkuu wa Shirika la Misri ili kupambana na dawa kulevya.


Hiyo ilitokea wakati wa Ushiriki wa Waziri wa Vijana na Michezo katika mikutano ya Bodi ya Usimamizi wa Ofisi ya Utendaji wa Wakala ya kimataifa ili kupambana na dawa za vichocheo, ifanyikayo huko mjini Monteryal ya Canada mnamo kipindi Novemba,17 -18, akizingatiwa kama mjumbe wa Bodi ya Usimamizi wa wakala ya kimataifa ili kukabiliana na dawa za kulevya (WADA).


Mkutano huo ulikuwa pamoja na juhudi za nchi za kiafrika ili kupambana na dawa za vichocheo misuli katika  Michezo, maendeleo yaliyofanywa na bara la Afrika kuhusu suala hilo kupitia nchi nyingi, zikiongozwa na Misri.


Inayotarajiwa ni kuwa mikutano ya Ofisi ya kiutendaji  ya wakala wa kimataifa ili kukabiliana na dawa za vichocheo inaangaza mafaili mengi ikiwemo kupima viashirio muhimu vya utendaji na kutathimini hali ya sasa ya mafanikio yaliyopatikana katika kiwango cha kupambana na vichocheo vya michezo katika nchi mbalimbali Duniani,pamoja na kuangaza kikundi cha masuala yanayohusiana na wanariadha na baadhi ya mashirikisho ya michezo ndani ya baadhi ya nchi.

Comments