Kamati kuu ya sayansi ya Wizara ya Vijana na Michezo yajadili programu na mahitaji ya mradi wa kitaifa wa Vipaji na Bingwa wa Olimpiki
- 2022-11-19 12:42:36
Kamati kuu ya Sayansi ya Wizara ya Vijana na Michezo inaongozwa na Dkt.Kamal Darwish ,ilijadili Programu zote na mahitaji ya mradi wa kitaifa wa Vipaji na Bingwa wa Olimpiki،haswa za awamu zake nne:- Wachipukizi, Juniors, Vijana na wasomi zinazoenezwa katika majimbo yote ya Jamhuri، vituo vya mafunzo ambavyo idadi yao ifikapo kama vituo 200 maalum.
Mkutano huo ulijadili jinsi ya kuandaa programu maalum kwa Lishe bora, afya ya kisaikolojia na programu maalum ya kisanaa, uchambuzi wa kimwili na kuangalia kuboresha utendaji kwa wachezaji wa mradi huo katika awamu zake zote.
Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo alisisitiza kwamba Kamati hiyo inalenga kuandaa Viwango na udhibiti maalum; kusaidia programu na Shughuli za taasisi ya michezo na malengo yake ya kila mwaka hadi Olimpiki ya mwaka wa 2024, sambamba na malengo ya Misiri katika sekta ya Michezo sawa na kufikia kilele, maendeleo ya michezo na dawa ya michezo.
Dkt Ashraf Sobhy aliashiria kuwepo ushirikiano moja kwa moja na baadhi ya mashirikisho ya michezo katika mradi huo kuhusu talanta na bingwa wa Olimpiki ambaye matunda yake yalionekana kupitia kuunganisha wachezaji wake kadhaa kwenye timu za vijana katika michezo ya Kunyanyua Uzani , Mieleka na Judu pamoja na usimamizi wa kamati maalumu ya kisayansi ya mradi huo.
Waliohudhuria mikutano hiyo ni :
viongozi wa Wizara ya Vijana na Michezo,meneja wa kiufundi wa mradi wa kitaifa ,Kundi la wataalam maalumu katika Sayansi na saikolojia ya mafunzo ya michezo na Kinesiolojia na sayansi ya lishe.
Ikumbukwe kama Mradi huo unatekelezwa kupitia idara kuu kwa vipaji wa mchezo kwenye sekta ya Michezo, pamoja na usimamizi endelevu wa Mkurugenzi Mkuu wa Vipaji vya Michezo,Mkuu wa idara kuu ya Utendaji wa Michezo na Msaidizi wa Waziri wa Masuala ya Mashindano.
Comments