Waziri wa Vijana na Michezo azungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Suez Canal


Dkt. Ashraf Sobhy asisitiza : Vijana wana msaada na uongozi wa siasa wenye hekima unaowaamini vijana....kwa vijana maendeleo yanahakikishwa ...na mustakbali wa nchi unaimarisha.

Kila ziara kwa Chuo Kikuu cha Suez Canal tunaona hatua thabiti kuelekea ubora, uongozi na mwanafunzi yuko kama kipaumbele chake.

Utamaduni wa kazi ya pamoja ni lazima kuwa pekee na kujumuisha watu wote.

Kumheshimu binti wa Shahidi kiongozi "Amr Waheb" kwa ubora wake wa riadha pamoja na kumpata ngao ya Wizara ya Vijana na Michezo.

Mkuu wa Chuo Kikuu anatangaza :Wizara wa Vijana na michezo ilikubaliana kuunga mkono Chuo Kikuu; kuanzisha  bwawa la kuogelea katika kitivo cha Elimu ya Kimwili , Chuo Kikuu cha Suez Canal.

Mnamo siku za kwanza uchaguzi wa wanafunzi...tulitoa kwa wanafunzi wetu maoni na mawazo ya Wizara ya Vijana na Michezo kutoa msaada kwa Vijana wa Chuo Kikuu.

Wanafunzi wanaojitolea kwa Chuo Kikuu cha Suez Canal wao ni mfano mzuri na wana mchango muhimu kuandaa mikutano yote ya wanafunzi.

Leo Alhamisi ,Dokta Naser Mandur, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Suez Canal,alipokea Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo kwenye makao  makuu ya Chuo Kikuu; kushiriki katika mkutano wazi  pamoja na Vijana wa Chuo Kikuu pamoja na "Vijana wa Jamhuri Mpya"

Wimbo wa kitaifa  kwa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri ulianza basi Dkt. Naseer Mandur alitoa kauli yake ambapo alimkaribisha na Waziri wa Vijana na Michezo;akitoa Shukrani kwake kwa kujali yake maoni msingi kwa kuboresha Vijana wa Vyuo Vikuu vya Misri,ambapo ni Waziri wa Vijana wa  kwanza kutoka vyuo vikuu vya Elimu ya Kimwili ,na mmoja wa maprofesa  mashuhuri katika Chuo Kikuu cha Helwaan,akisifu duru yake kuunga mkono kuimarisha vituo vya vijana,na mawazo yake  yanayochanganya kitaaluma na kutumika na duru yake katika kutoa msaada kwa kitivo cha Elimu ya kimwili kwa kubaliana kuanzisha bwawa lako la kuogelea.

Aliwahutubia wanafunzi kwamba ni lazima kuwa na sifa nzuri za maadili,akieleza kwamba Jambo kuu la mafanikio ni kuweka malengo  wazi kukabiliana na changamoto ndani na nji.

Kupitia  mazungumzu yake kati ya wanafunzi, Dkt. Ashraf Sobhy alisisitiza kuwa pamoja na mwanzoni wa Jamhuri mpya ,Taasisi zote za serikali kwa Vijana na uwekezaji, kujenga huanza na wao kuelewa matumaini na mustakbali,akiongeza kwamba taifa hushuhudia sasa Mafanikio kadhaa katika sekta zote, miradi ya mji mpya na kuboresha miundombinu yanafungua fursa mbalimbali za kazi kwa vijana ni inaitwa ufunguzi wa Uchumi.

Waziri alisifu maendeleo ambayo sekta ya elimu inashuhudia na kuanzisha mashirika yasiyo ya vyuo vikuu yanayojumuisha nyanja mbalimbali kwa watu wote, akisisitiza kwamba kipindi cha chuo Kikuu ni bora kuliko vijana katika  maisha ya vijana,na ni lazima kuna shughuli mbalimbali kuongeza Ujuzi na Sifa za kibinafsi kwa mwanafunzi na kujali misingi na maadili ya maadili kama Heshima،,Uzalendo, Mfano mzuri.

Dkt. Ashraf Sobhy aliongeza kwamba Wizara ya Vijana na Michezo ina mirada na mipango kadhaa ambayo ulilenga kufichua talanti kwa kushiriki pamoja na wizara ya Elimu ya Juu, mifano; sherehe ya "ubunifu" kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Misri ni mashindano maarufu ya ubunifu zaidi kwa Vijana pamoja na kuanzisha vituo vya sanaa vingi ndani ya Vyuo Vikuu.

Pia alisifu mafanikio ambyo Chuo Kikuu cha Suez Canal hushuhudia, ikiongozwa na Nasser Mandur ingawa ni Chuo Kikuu kipya lakini ni kina hatua thabiti kuelekea ubora na kuweka mwanafunzi katika kipaumbele chake.

Mwishoni mwa semina hiyo ,Mchezaji Malak Amr Wahib,mwanawe wa shahidi Meja Amr Wahib na ambaye alishinda nafasi ya kwanza kwenye ubingwa wa Jamhuri ya mazoezi wa viungu vya mwili, Waziri alimtoa ngao ya Wizara ya Vijana na Michezo.

Waziri huyo na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Suez Canal walichukua picha ya ukumbusho pamoja na familia ya wanafunzi wa mpango wa kwa ajili ya Misri ,na Timu ya kujitolea ya  Chuo Kikuu cha Suez Canal.

Dkt.Kamal Darwish, Mwenyekiti wa kamati ya Kisayansi katika Wizara ya Vijana na Michezo,Mkuu wa zamani wa Kitivo cha Michezo katika chuo kikuu cha Helwan,Dokta.Heussin Alsamri, Mwenyekiti wa Sekta ya Elimu ya michezo ya baraza kuu katika vyuo,Dkt.Arafa Salama, mwenyekiti wa Shirikisho la Michezo vyuoni,Dkt.Sobhy Hasanin, Naibu mkuu wa Shirikisho la Michezo ya Misiri vyuoni,Dkt.Fathi Nda, Kapteni wa taaluma za Michezo,Sami. Abd- Alhalim, Mkuu wa Mkurugenzi wa Vijana na Michezo katika mkoa wa Alismailia, walimu wa vyuo vya Elimu ya Michezo katika jamhuri ya Misri na kundi la viongozi vya michezo wote walihudhuria mkutano huu.


Na kutoka Chuo Kikuu Dkt.Muhamed Abd Alnaim, Naibu mkuu wa Chuo cha Mambo ya Elimu na Wanafunzi,Dkt.Muhamed Sad Zaghlul, Naibu mkuu wa Chuo cha Masuala ya Elimu ya juu na Tafiti,Bi.Hoda Farg Amin,mkuu wa chuo, Dokta.Maged Al-Aradhi,Mkuu wa Elimu ya Michezo na wakuu wengine wa Vyuo na wajumbe wa kamati ya mafunzo ya Chuo Kikuu walihudhuria mkutano pia 

Dkt.Muhamed Ghanim, mratibu mkuu wa shughuli za wanafunzi, Dkt.Muhamad Al-Baz, Mratibu wa familia ya wanafunzi wa mpango wa kwa ajili ya Misri, walisimama uratibu wa mkutano.

Comments