Wizara ya Vijana na Michezo yazindua Mkutano wa Pili kwa Viongozi wa Vijana wa Vyombo vya Habari Ulimwenguni mwa Kiarabu


 Pamoja na Ufadhili wa  Mheshimiwa Rais wa Jamhuri, Rais Abdel Fattah El-Sisi, Wizara ya Vijana na Michezo inazindua Matukio ya Mkutano wa Pili kwa Viongozi vya Vijana wa Vyombo vya Habari katika Nchi za Kiarabu mnamo Februari ijayo, hivyo kupitia Idara Kuu kwa Elimu ya Uraia ( Utawala wa Umma wa Ukarabati wa Kada za Vijana ) na Utawala wa  Mahusiano ya Umma na Vyombo vya Habari.


Vijana, wanafunzi, washiriki wa kitivo kama wanachuoni na wenye shahada ya uzamili kwenye vitivo na vitengo vya vyombo vya habari na mawasiliano na nyaraka nchini Misri na nchi tofauti za kiarabu, wanashiriki katika mkutano.


Mkutano huo unakuja ndani ya mfumo wa kubadilika uzoefu, maoni, majaribio ya mafanikio kati ya viongozi vya vijana wa vyombo vya habari kutoka kwa Misri na wenzao kwenye ulimwengu wa kiarabu, kuunganisha ushirikiano na kuchangia katika kuweka misingi na ramani ya njia ya vijana vya vyombo vya habari ambayo inaimarisha maadili ya utambulisho na utamaduni wa kiarabu.


Inatajwa kwamba Wizara hiyo imeandaa toleo la kwanza kutoka mkutano wa viongozi wa vijana wa vyombo vya habari  ndani ndani kwa ushirikiano wa vijana na wanafunzi wa vitivo na vitengo vya vyombo vya habari katika vyuo vikuu vya Misri na wanafunzi 160 wa kiume na wa kike kutoka  kwa vituo vikuu 36, vyuo na akademia pamoja na vijana vya vyombo vya habari, vijana vya vyama na wanasiasa.

Comments