Waziri wa Vijana na Michezo akutana na Mkuu wa FIFA katika Mechi ya Kombe la Dunia la Tunisia na Ufaransa nchini Qatar


Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo amekutana na Gianni Infantino ambaye ni Mkuu wa  Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu"  AL FIFA", hivyo pamoja na uwepo wake katika mechi ya Ufaransa na Tunisia, miongoni mwa mashindano ya kombe la Dunia yanayokaribishwa na Qatar.


Mkutano huo ulifanyika kwa uwepo wa  Amr El- sherbiny, Balozi wa Misri huko  Doha, na Mhandisi Hani Abu Raida, Mjumbe wa Ofisi ya kiutendaji kwa FIFA.


Mkuu wa FIFA ameukaribisha uwepo wa Waziri wa Vijana na Michezo Dokta, Ashraf Sobhy, kwa idadi kadhaa za mechi za kombe la dyunia nchini Qatar ndani ya mfumo wa mwaliko rasmi iliyotolewa kwa maafisa kutoka nchi mbalimbali Duniani.


Kwa upande wake, Waziri wa Vijana na Michezo ametoa Shukrani kwa kiwango cha mashindano yaliyoshuhudiwa na ubingwa wa kombe la Dunia, na mwonekano wa kipekee kwa timu mbalimbali katika jukumu la makundi, akizitakia mafanikio katika hatua zifuatazo za ubingwa ambayo unayopata ufuatiliaji na ujali wa nchi zote za Dunia.

Comments