Wizara ya Vijana na Michezo na Shirika la Kazi la Kimataifa yashiriki katika meza moja ya kuwaunganisha Wamisri na Wakimbizi kwa Ufundi wa Soko la Ajira la Kimisri


Wizara ya Vijana na Michezo ikiwakilishwa idara kuu ya kuwawezesha vijana imeshiriki katika meza ya pande zote  ili kujadili mapendekezo ya kurahisisha kuwaunganisha wamisri na wakimbizi kwa ujuzi katika soko la ajira la Misri, ambayo iliandaliwa na Shirika la kazi la Kimataifa kwa ushirikianao na kikundi cha washirika wanaohusika wa masuala ya wakimbizi nchini Misri, kwa uwepo wa Manal Gamal  Al_Din, katibu wa Wizara na Mtawala wa Idara Kuu ya uwezeshaji vijana ndani ya Wizara ya Vijana na Michezo.


Kikao hicho cha majadiliano  ni sehemu ya mazungumzo ya kijamii yaliyopo kati ya washirika wa mradi, wenye uamuzi wakuu na wanaohusika na masuala ya wakimbizi na wahamiaji ili kubadilishana ujuzi na kufikia kwa mapendekezo ya kuboresha hali hii, na kuchangia katika kuwajiunga wakimbizi na wahamiaji katika kazi rasmi ambazo zinazingatia  sheria na kanuni za Misri, ambayo husababisha kuboresha hali ya kiuchumi na maisha ya watu husika, aidha maendeleo ya kiuchumi kwa nchi, na kujadili mihimili ya kuweka mkakati wa pamoja ili kuandaa uingiaji wa wakimbizi katika soko la ajira.


Kikao hicho cha majadiliano kinatokea ndani ya shughuli za mradi wa vilabu vya kutafuta kazi vya " Vijana kwa kesho"unaolenga kuandaa vijana kuhusu jinsi ya kupata nafasi nzuri ya kazi, na kuwaunganisha tena vijana waliyokuja kutoka nje, na kutambua changamoto zilizowakabili katika soko la ajira la Misri.


Kwa upande wake, Manal Gamal Al_Din, amesisitizia umuhimu wa kuwaunganisha wakimbizi na wahamiaji pamoja na wamisri ndani ya shughuli zote na programu zilizotekelezwa kupitia Wizara ya Vijana na Michezo, akiashiria nia ya Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, kwa kujali na jambo hilo.


Ikumbukwe kwamba mradi unalenga kuandaa vikundi vya vikao vya mazungumzo ili kuweka siasa maalumu kwa ajili ya kupambana na changamoto za kuwaunganisha wahamiaji, kudhibiti mfumo wa kikanuni na kisheria maalumu ya mbinu za kupata nafasi nzuri ya kazi  katika makampuni ya sekta binafsi.

Comments