Waziri wa Michezo apokea Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Squash


Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo amempokea Zina Waldridge, Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Squash katika Makao Makuu ya Wizara kwenye Mji Mkuu Mpya wa Utawala, ili kuangazia njia za ushirikiano pamoja na shirikisho la kimataifa la Squash.



Mkutana huo ulikuwa pamoja na uwepo wa Dkt. Assem Khalifa, Mkuu wa Shirikisho la Misri la Squash,  Karim Darwish, Makamu wa Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Squash, na William Lewis Marie Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Kimataifa la Squash.


Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo ametoa Shukrani kwa Mkuu wa Shirikisho la kimataifa la Squash nchini Misri, akiashiria kwamba mchezo ya Squash unashuhudia kushamiri kwa michezo na ujenzi nchini Misri, aidha mabingwa wa Misri wanaendelea kuongeza katika uainishaji wa kimataifa wa Squash na kushinda mataji ya Dunia, hivyo vyote ni kulingana na uungaji mkono na usaidizi mkubwa ambao Misri inaupata, na kutoa nafasi za mafanikio ili kuendelea kwao.


Akiongeza kwamba Wizara ya Vijana na Michezo inatoa juhudi kubwa pamoja na  ushirikiano wa mashirika ya kiraia na sekta binafsi, ili kuwasaidia mabingwa na nchi za Misri ili kuboresha kwa michezo ndani yake.


Waziri huyo ameashiria kwamba kuna zaidi ya vituo 5000 vya Vijana nchini Misri, pia kuna viwanja vingi vya Squash katika mikoa mbalimbali, ambapo amegundua kwamba vijana vya Misri wanataka kucheza Squash, si katika mkoa wa Kairo tu, bali katika mikoa mingine, sababu ya umaarufu na utashi inayopatwa na vijana vya Misri.



" Tunfurahi kwa ushirikiano wa shirikisho la kimataifa la Squash, ambapo tumegundua mambo mengi yaliyokubaliwa kwa maafikiano ya maoni na mtazamo, tunatamani zaidi mnamo siku zijazo kwa ajili ya kuboresha michezo nchini Misri", Waziri wa Vijana na Michezo amesema hayo alipohitimisha  hotuba yake.



Zina Waldridge, Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Squash, anaonyesha mshangao wake kwa uboreshaji na maendeleo makubwa ambazo Misri inashuhudia, katika suala la ukuaji wa ujenzi wa miundombinu ya vilabu na viwanja vya Squash.


Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa ameeleza ufahamu wake, kwa nini Misri inataka kuendelea ili kuandaa Mchezo ya Olimpiki, ambapo aliweka mpango mwema na uliwekwa kwa uangalifu, ambayo ni ishara nzuri ya uwezekano wa kufaulu kwa faili ya kimisri katika kuandaa Mchezo ya Olimpiki mwaka 2034.


 Pia ametoa Shukrani kwa jukumu kubwa la Wizara ya Vijana na Michezo katika kueneza utamaduni wa michezo nchini Misri kwa ujumla na haswa Squash, akisisitiza kwamba anafuatilia yanayotokea nchini Misri ya vivutio vingi vya kufanya michezo kama  " Tamasha la Mbio Marathon na Baiskeli" ambayo huwavutia vijana kushiriki katika matukio kama hiyo, akieleza kuna ripoti kuhusu Squash imetaja kwamba mchezo wa Squash ni " mchezo wa afya zaidi kati ya michezo mingine yote"


Ni vyema kutaja kwamba Misri ni mwenyeji wa michuano ya timu ya Dunia ya Squash ya wanawake kwa timu, kuanzia 10 hadi 16 Desemba hii, ambapo timu ya taifa ya wanawake inayojumuisha "Noran Johar, Nour El-Sherbiny, Hania El-Hamami na Nour El-Tayeb" wamefikia robo fainali ya michuano, 

baada ya kuwashinda wanawake wa Canada  3- 0  jana, kuwaongoza wanawake wa timu ya kitaifa katika kundi la kwanza.

Comments