Ni uwanja
wa rasmi ya timu ya soka ya Misri.
Uwanja huo ulianzishwa mwaka 1958 katika zama za Rais wa Misri, Gamal Abdel Nasser, kwa jina la uwanja wa
Nasser.
Uwanja huo
ulishuhudia Kombe la Kimataifa la Afrika
mwaka 2006, ambapo Misri
ilishinda kombe hili , pia Michuano ya Kombe la Dunia Chini ya Miaka 20
ilifanyika uwanjani humo katika mwaka 2009, uwanja huu unaweza kukusanya hadi
watazamaji 75,000.
Uwanja wa
Kimataifa wa Kairo ni uwanja wa kwanza
wa aina yake na uwanja wa Olimpiki katika Mashariki ya Kati na Afrika ambao uko
katika Mji wa Nasr (Nasr City) ,
kaskazini mashariki mwa kairo.
Uliundwa
na mhandisi wa Ujerumani Werner Mars, mhandisi huyo ndiye aliyeunda Uwanja wa
Olimpiki huko Berlin. Ulikamilishwa mwaka wa 1960, ulifunguliwa na Rais
marehemu Gamal Abdel Nasser katika sherehe ya Mapinduzi ya Julai mwaka huo huo.
Mwaka wa
2005, uwanja wa Kairo umerekebeshwa ili ufanane na Uwanja wa Olimpiki mpya
katika karne ya 21, ambapo ulikuwa mwaka wa Kombe la Kimataifa la Afrika ya
2006. Uwanja huo uko mbali na Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa kairo kwa masafa ya kilomita 10 na kilomita 30
kutoka Katikati ya mji wa Kairo.
Miongoni
mwa marekebesho ya uwanja kuna majengo kadha yanayoanzishwa kama mji wa
michezo; kwa mtiririko huo:
kambi wa beseni.
Jumba yaliyofunikwa.
Uwanja wa Mafunzo (mpira wa mikono - Mpira wa kikapu –
voliboli – tenisi - Mpira wa vinyoya ).
Uwanja wa Hoki.
Uwanja wa farasi : Unahusisha Shirikisho
la Kimataifa la farasi - eneo la gorofa la mita za mraba 15942 ardhi ya michezo ni mita za mraba 73 x 138.
Jumba ya boga : jumba inajumuisha uwanja wa
michezo kuu na (uwanja nne) kwa mafunzo
.
Viwanja vya michezo vya mpira wa miguu:
Viwanja nne vya soka
Ukumbi wa wazi : vifaa vya kupokea
mikutano, sherehe na maonyesho ya michezo, ulizinduliwa tarehe 14 Novemba 1984
na Rais Mohamed Hosni Mubarak juu ya eneo la 76552 m2.
Uwanja wa Kimataifa wa farasi
(unaoendelea) Uwanja wa baiskeli wa Kimataifa (chini ya
ujenzi).
Shughuli
za marekebesho na maandalizi ya uwanja wa kimataifa wa kairo zinaendelea siku
hizi katika majaribio ya kuandaa uwanja huo ili kuikaribisha michuano ijayo .
Michuano itakayofanyika nchini Misri katika kipindi cha 13 juni hadi 21 julai
mwaka 2019 . Kwa hivyo watekelezaji wanafanya juhudi zaidi , ili kutimiza
shughuli za marekebesho ya uwanja kwa mfumo unaoonesha uwezo wa nchi juu ya
kupanga na kuikaribisha moja kati ya michuano mikubwa ulimwenguni.
Comments