Waziri wa Vijana na Mkuu wa Mkoa wa Alexandria wawatawaza washindi wa Zayed Charity Marathon katika Uwanja wa Kimataifa wa Alexandria, Pamoja na Ulinzi wa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El_Sisi


Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, na Jenerali Muhammad Al-Sharif, Mkuu wa Mkoa Alexandria, wamewatawaza Washindi wa Zayed Charity Marathon, ambayo hutekelezwa na Wizara Kupitia Idara Kuu ya Maendeleo ya  Michezo( Utawala wa Umma), na mapato kutoka kwake yametengwa kwa Hospitali ya Ahl Masr kwa matibabu ya bure ya waathirika wa moto, mbele ya Uwanja wa kale wa Alexandria.       


 Washindi katika mbio ya wenye ulemavu kwa wanawake ,ameshinda katika nafasi ya kwanza Huda Ahmed, nafasi ya pili Amal Abdel Aziz na nafasi ya tatu Sama Ayman Haddad. Na miongoni mwa  wenye ulemavu kwa wanaume, ameshinda katika nafasi ya kwanza Walid Jaber, nafasi ya pili Haitham Adel na nafasi ya tatu Muhammad Rashad. 


wanawake washindaji katika mbio kuu katika nafasi ya kwanza ameshinda Amina Bakhit, nafasi ya pili Basmala Abdel Hamid na nafasi ya tatu Jihad Mustafa, ama kwa wanaume, ameshinda katika nafasi ya kwanza  Muhammad Salem, nafasi ya pili  Noureddine Abu Bakr na nafasi  ya tatu Abdullah Adel, huku zawadi zilizosalia zitatumwa kupitia barua ya Misri kwa kila mshindi.


Tuzo zinazotolewa kwa washiriki katika mbio zinafikia takriban paundi milioni tano, ambapo tuzo zitagawiwa kwa washiriki elfu tano, kama idadi kubwa zaidi ya tuzo ambazo zitawasilishwa kwa washindani katika moja ya mbio kubwa za michezo, mapato ya Zayed Charity Marathon katika toleo lake la saba yametengwa kwa Hospitali ya Ahl Masr kwa matibabu ya bure ya waathirika wa moto, pamoja na kufanya bahati nasibu ya umma ili kuchagua  washiriki sitini  kwa ajili ya safari ya Umrah.



Washindi hao wametawazwa  mbele ya Luteni Jenerali Muhammad Hilal Al Kaabi, Mkuu wa Kamati Kuu ya Maandalizi ya mbio za Zayed Charity Marathon, pamoja na ujumbe alioandamana naye, Luteni Jenerali Ashraf Atwa kamanda wa Vikosi Vya wanamaji, Balozi Maryam Khalifa Al Kaabi,  Balozi wa Umoja wa Falme za Kiarabu nchini Misri, Dkt. Heba El Sewedy,  mwanzilishi na mkuu wa Bodi ya Wadhamini ya Wakfu wa Maendeleo wa Ahl Masr, Kundi la Viongozi wa Wizara ya Vijana na Michezo, Nyota wa Sanaa, wa Michezo, wa Media, pamoja na Ushiriki wa mamlaka mbalimbali zinazohusika, Hilali nyekundu  ya Imarati na ya Misri,  wadhamini wa sherehe hiyo, na Kampuni ya  Kairo Runners  inayoandaa sherehe hiyo.

Comments