Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alifanya mkutano mkubwa na wakuu na wawakilishi wa mashirikisho 22 ya michezo na wawakilishi wa kampuni na taasisi kadhaa za kibinafsi kujadili maandalizi ya mwisho ya uanzishaji wa Maonesho ya Kimataifa Sports Expo, pamoja na Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri.
Inatarajiwa kwamba Maonesho hayo yataanza Februari 22, 2023 katika Kituo cha Mikutano ya Kimataifa cha Al-Manara na yatakaofanyika kwa muda wa siku nne.
Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alisisitiza kuwa maonesho hayo ni moja ya matokeo muhimu zaidi ya mwamko wa michezo ambao Misri inashuhudia kwa sasa katika nyanja mbalimbali.
Inapangwa kwamba Maonesho ya Kimataifa Sports Expo yatashuhudia maelezo yote ya maendeleo na miradi ya mwamko wa michezo katika mfumo wa michezo wa Misri kwa ujumla, ambapo maonesho yatajumuisha mabanda mengi yanayojumuisha ushiriki wa mashirikisho yote ya michezo ya Misri na vilabu vya michezo na mawasilisho na michango ya mamia ya makampuni na taasisi za michezo nchini Misri, Nchi za Kiarabu na za kigeni katika masuala ya michezo na vifaa vya michezo.
Pia imepangwa kuwa maonesho hayo yatajumuisha utekelezaji wa shughuli nyingi zitakazofanyika kando ya matukio makuu, ikiwa ni pamoja na mkutano wa kisayansi, ambao Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Shirikisho la Misri na wanaohusika wote na wataalamu wa masuala ya michezo, pamoja na semina kadhaa na warsha za kupitia muundo wa michezo na vijana wa Misri na uwezo wa Misri katika kuandaa matukio makubwa ya michezo ya kimataifa na kutambulisha uwezo mkubwa wa Misri katika uwanja huu.
Siku zijazo zitashuhudia kufanyika kwa mikutano mingi inayohusika na kukamilisha kazi za mwisho za maonesho na shughuli zake mbalimbali .
Comments