Waziri wa Vijana na Michezo atafutia pamoja na Waziri wa Vijana wa Australia kuamsha hali ya ushirikiano wa pamoja


Sobhy.. alionesha nafasi mbalimbali kwa ushirikiano pamoja katika nyanja mbalimbali haswa kwenye nyanja za wachipukizi na Vijana.


Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo alifanya mkutano wa mtandaoni pamoja na Dkt. Ann Ali, waziri wa Vijana wa Australia, kwa mahudhurio ya Balozi Mahamud Zaid,balozi wa Misri nchini Australia kutafuta njia za ushirikiano pamoja na nchi hizo mbili.

Mkutano uliangazia  ushirikiano pamoja na kuratibu mkataba wa makubaliano katika nyanja mbalimbali miongoni mwa "kuanzisha kikao cha kiutamaduni kati ya Vijana wa Misri na Australia, Ujasiriamali, mipango haswa Jumuiya ya Misri nchini Australia, mipango ya walemavu, ufadhili wa Nasser, mipango ya pamoja,ubadilishaji wa uzoefu katika nyanja kadhaa nyingine"

Waziri huyo alipongeza  Dkt. Ann kushika madaraka ya Wizara ya Vijana nchini Australia, akielezea furaha yake kwa mwenye asili ya Misri kupata nafasi hiyo , akisisitizia kuwa Vijana wa Misri wana uwezo mwingi unaowasaidia kutawaliwa nafasi za uongozi kadhaa Duniani.

Na pia alipongeza kwa mafanikio ya faili ya Australia kupata uandaaji wa Michezo ya Olimpiki mwaka wa 2032 ,pia uratibu wa pamoja na New Zealand kuandaa Kombe la Dunia la Wanawake la FIFA katika toleo la tisa, mwaka wa 2023, kwa  kushiriki timu 32 kutoka Kombe la Dunia ambalo litazinduliwa Julai ijayo.


Waziri wa Vijana alionesha kwamba mahusiano ya Misri ya Australia yanapanuliwa,na kuna matarajio kadhaa na tamaa ya ushirikiano katika nyanja mbalimbali,hivyo Wizara ya Vijana na Michezo ilitafuta kufaidika ili kukuza mahusiano  kwa pande kati ya Vijana wa Misri na Australia na pia kuanzisha mipango kadhaa kwa jumuiya ya Misri nchini Australia na ufahamu wa vijana kuhusu umuhimu wa nchi yao miongoni mwa mipango ambayo Wizara inayoifanyia kazi na imepangwa kwa kwa kusudi hili.

Na pia Dkt. Ann Ali, Waziri wa Vijana wa Australia alitoa shukrani kwa Waziri wa Vijana na Michezo kwa  juhudi zake za kuanzisha mkutano muhimu huu, unaozingatiwa hatua muhimu kuzidisha miradi mbili kati ya nchi mbili katika nyanja mbalimbali haswa nyanja ya Vijana,akionge,a kusisitiza umuhimu wa maendeleo ya ushirikiano pamoja na nchi ya Australia na Misri kwani Misri ina duru ya kiuongozi na muhimu kubwa katika nyanja mbalimbali.

Na pia alisisitiza kwamba ana fahari kuwa Mmisri na alipata elimu yake nchini Misri,aliweza kufikia nafasi yake ya kisasa, haswa na alimaliza masomo yake katika awamu ya chuo kikuu nchini Misri ambayo ina athari kubwa katika maisha yake.

Aliongeza kwamba jumuiya ya Misri nchini Australia na kubwa na huko kuna Vijana wa kizazi cha pili na cha tatu walitaka kujua kuhusu nchi yao mama, Misri .hivyo umuhimu wa ushirikiano ambayo utakaofanyika na Wizara ya Vijana na Michezo ya Misri haswa katika mipango vijana wa Australia kuhusu ubadilishaji wa Vijana .

Akibainisha kwamba toleo la mwisho la "Udhamini wa Nasser" lililofanyika katika toleo la tatu , vijana wengi  wa Australia walishiriki  humo ,ambao walionesha furaha yao ya kushiriki baada ya  kuhamisha vizuri uzoefu waliojifunza katika udhamini huo kwa wenzao baada ya kurudi.

Waziri wa Vijana alihitimisha maeneno yake kuandaa ziara ya Misri kufanya mkataba wa pamoja.

Kwa upande wake Balozi wa Misri nchini Australia Mahamud Zaid,alitoa shukrani kwa Waziri wa Vijana na michezo kwa juhudi zake kwa ajili ya kukuza mahusiano kati ya nchi mbili,na pia kwa jumuiya ya Misri nchini Australia na  kurudisha mawasiliano Kati ya Vijana na nchi yao mama.

Comments