Waziri wa Vijana na Michezo aunga mkono timu ya Misri kwa Vijana


Waziri wa Vijana na Michezo, Dkt. Ashraf Sobhy, alitembelea kambi ya timu ya Misri kwa Vijana, kuisaidia timu hiyo kabla ya makabiliano yajayo na timu ya Nigeria kesho, Jumatano, katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa Umri wa chini ya miaka 20. 


Mkutano huo ulihudhuriwa na Mahmoud Gaber, Mkurugenzi wa kiufundi kwa timu hiyo, wafanyakazi wa kiufundi na kiidara kwa timu hiyo, na wanachama wa Shirikisho la Soka la Misri: Meja Jenerali Helmy Mashhour na Kapteni Hazem Imam, pamoja na Dkt. Mohamed Al-Kurdi, Mkuu wa Idara Kuu ya kiutendaji wa Michezo katika Wizara ya Vijana na Michezo. 


Waziri huyo wa Vijana na Michezo amewahamasisha wachezaji wa timu ya Misri kwa Vijana kufanya kila liwezekanalo kufikia hatua inayofuata na kutwaa ubingwa huo utakaofikisha zamu kwa fainali za Kombe la Dunia nchini Indonesia kuanzia Mei 20 hadi Juni 11. 


Waziri huyo wa Michezo amegusia ushirikiano wa wizara hiyo na Shirikisho la Soka nchini ili kufanikisha maendeleo yanayotakiwa katika ngazi ya timu za taifa, na kuonekana katika taswira nzuri katika mashindano mbalimbali yajayo na kuwafurahisha mashabiki wa Misri wanaosubiri wachezaji wengi wa timu za mpira wa miguu katika mashindano yajayo.


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa kiufundi wa timu ya Misri kwa Vijana aliahidi kupita hatua ya makundi, kupanda na kufanya vizuri. 


Leo, kocha wa timu ya kwanza ya Soka ya Misri, Rui Vitoria, aliwaunga mkono vijana wa Mafarao, akiwataka wacheze kwa ajili ya kuweka historia. 


Timu hiyo ya Misri ipo kundi A pamoja na Senegal, Nigeria na Msumbiji huku kundi B likishirikisha Congo, Uganda, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Sudan Kusini huku Benin, Zambia, Gambia na Tunisia zikishiriki kundi C.

Comments