Waziri Mkuu akutana na Mkuu wa CAF kutathmini njia za kusaidia Soka Afrika


Waziri Mkuu Dkt.Mostafa Madbouly amekutana jioni ya leo na Patrice Motsepe, Mkuu wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), ambapo walipitia mada kadhaa muhimu zinazolenga kusaidia Soka la Afrika, haswa kutokana na maendeleo makubwa iliyoshuhudiwa mnamo siku za hivi karibuni.

Mkutano huo ulihudhuriwa na Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo na Veron Mosengo Omba, Katibu Mkuu wa CAF.

Waziri Mkuu alianza mkutano huo kwa kumkaribisha Rais wa CAF, akisema: “Napenda kutumia fursa hii kuelezea uungaji mkono kamili wa Misri kwa mipango ya CAF inayolenga kuendeleza Soka la Afrika na kusaidia uwepo wa Afrika katika matukio ya kimataifa ya michezo.”

Aliongeza kuwa viwango vya utendaji tulivyoshuhudia wakati wa Kombe la Dunia lililopita nchini Qatar vinaakisi kiwango Soka la Afrika lilivyooendeleza, akisifu utendaji wa timu za Afrika, haswa Morocco. Pia alisisitiza kuwa Misri iko makini kutoa aina zote za msaada na Udhamini ili kuendeleza mfumo wa Soka Barani Afrika ili kuendeleza maendeleo yake ya kisasa.

Waziri Mkuu alieleza kuwa Misri pamoja na taasisi zake zote inaangalia faili la michezo kwa maslahi makubwa, akiashiria uzoefu mashuhuri wa taifa la Misri katika kuandaa matukio mengi makubwa ya michezo ya kimataifa, haswa mashindano ya Soka ya Afrika na Kombe la Dunia la Mpira wa Mikono.

Madbouly alisisitiza utayari wa Misri kuandaa mashindano makubwa ya michezo na matukio, kwa kuzingatia umiliki wake wa miundombinu na vifaa vya michezo kwa mujibu wa vipimo na viwango vya kimataifa, kwani ilianzisha Jiji la Kimataifa la Misri kwa ajili ya Michezo ya Olimpiki kwenye eneo la ekari 450, na ina uwanja wa michezo wenye uwezo wa viti 92,000, viwanja, viwanja vya michezo na hoteli, kwani mji huo uko katika eneo la kimkakati linalounganisha idadi ya magavana na miji, ambayo ni Kairo, Suez, Ain Sokhna na Mji Mkuu wa Utawala.

Wakati wa mkutano huo, Mkuu wa Shirikisho la Soka la Afrika aliishukuru serikali ya Misri na watu kwa kuwa mwenyeji wa makao makuu ya CAF, akielezea matumaini yake kwamba kipindi kijacho kitashuhudia ushirikiano zaidi kati ya serikali ya Misri na CAF ili kujenga kasi ya kihistoria ya uhusiano wa pamoja kati ya Misri na Shirikisho la Soka Afrika.

Katika mkutano huo, pia walijadili mipango ya CAF ya kuanzisha makao makuu mapya ya Muungano katika eneo la Kairo Mashariki.

Comments