Kulingana na tukio la kukaribisha mataifa ya Afrika: Kamati ya Utalii inatoa kampeni ya michuano kwenye nchi yako .. Tushirikishe mafanikio.

Chini ya kichwa cha "Michuano kwenye nchi yako....  Tushirikishe mafanikio", Kamati ya Shughuli za Utalii ndani ya  kamati iandaayo ya michuano ya Mataifa ya Afrika kwa Soka yanayokaribishwa kwa Misri kuanzia Juni 21 hadi Julai 19, itatoa kampeni ya ufahamu kwenye  mitandao ya kijamii ili kuhimiza umma wa Misri kushiriki kikamilifu katika mafanikio ya michuano hiyo.

 

Kampeni hiyo ina jukumu la   kuhamasisha  au kuwaita mashabiki ili  kueneza tabia chanya, kuanzia   kuwapokea watalii kwa tabasamu wakati wanapofika kwenye viwanja vya ndege vya kimisri, kuelekea  tabia chanya  kama vile usafi wa maeneo ya kiutalii, na kujitolea kwa nguvu kuhamasisha timu ya kitaifa na timu zinazoshiriki, na kuunga mkono kwa wazo la kadi ya mashabiki.

 

Kamel Abu Ali, mwenyekiti wa kamati ya shughuli za kiutalii, alisema kuwa kamati imeandaa mpango kamili wa kukuza maeneo ya kiutalii ya kimisri, na kuahidi ustawi wa ajabu wa  kiutalii  wakati wa michuano.Akifafanua kuwa Kamati ya Utalii katika michuano haijali maeneo ya kiutalii tu,  lakini inahangaika  kubadili utamaduni wa kuwapokea wageni.

Comments