Udhamini wa Nasser wakuza Bara Duniani...Sambamba na Maadhimisho ya Miaka 60 ya kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika
- 2023-06-07 10:53:48
Dkt.Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo wa Misri alisema: “Sambamba na maadhimisho ya miaka sitini ya kuanzishwa kwa Umoja wa Nchi Huru za Afrika (Umoja wa Afrika sasa), na maandalizi ya kuzindua toleo la nne la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, ambalo limepangwa kufanyikwa Juni hii ya 2023, ambalo ni muendelezo wa juhudi za taifa la Misri, katika kutekeleza jukumu lake lililopewa katika kuimarisha nafasi ya vijana ndani, kikanda, Barani na kimataifa kwa kutoa aina zote za usaidizi, kuwezesha na mafunzo, kwa kuzingatia Ajenda ya Afrika 2063 kama mojawapo ya nyaraka za bara ambalo Udhamini huo unategemea.
Vilevile Waziri huyo alielezea kuwa bara la Afrika mnamo kipindi cha miaka minne ndilo maarufu zaidi kwa Udhamini huo, akieleza kuwa toleo la kwanza lilizinduliwa kwa ushiriki wa Waafrika 100%, kisha Udhamini huo uliongezeka katika toleo lake la pili kwa kauli mbiu ya " Ushirikiano wa Kusini_Kusini”, kwa kupokea vijana wa Asia na Amerika ya Kusini, na bado Afrika ilirekodi idadi kubwa zaidi Idadi ya waombaji iliongezeka kwa takriban 56.7%, kisha idadi ya Vijana waafrika kupata Udhamini wa Nasser katika toleo lake la tatu mnamo 2022 iliongezeka hadi kufikia. takriban 84.6%, huku takwimu zikithibitisha kuwa licha ya nchi zipatazo 93 Duniani kwa Udhamini wa Nasser mwaka huo kama sehemu ya maandalizi toleo la nne, asilimia ya waombaji wa Kiafrika ilifikia takriban 84.7% ya jumla ya waombaji.
Comments