Wizara ya Vijana na Michezo yapokea idadi ya wajumbe Vijana wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, toleo la nne
- 2023-06-07 10:55:00
Wizara ya Vijana na Michezo, ikisimamiwa na DKT.Ashraf Sobhy ilipokea idadi ya wajumbe Vijana wanaoshiriki katika toleo la nne la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, ambao uko na Ufadhili wa Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri , kwa ushiriki wa viongozi vijana 150 wenye taaluma muhimu zaidi na tofauti tena vijana wanaoacha athari kubwa na wanashawishi katika Jamii ya kiraia Duniani kote.
Na DKT.Ashraf Sobhy, Waziri huyo wa Vijana na Michezo ameshasisitiza kuwa Udhamini huo umekuwa na makini ya kukuza nafasi ya Afrika na ifanyike iwe juu kabisa Duniani kote, ambapo Udhamini wa Nasser umezinduliwa katika toleo lake la kwanza mnamo Juni 2019 kama Udhamini wa (Kiafrika-Kiafrika) kwa ushiriki wa vijana takriban kutoka kwa nchi 28 za kiafrika na hiyo ilikuwa sambamba na Urais wa Misri kwa Umoja wa Afrika, na upanuzi na ushawishi wa Udhamini huo umepanuka hadi ukafika takriban nchi 93 Duniani kote, miongoni mwao nchi 49 za kiafrika,akielezea kuwa Udhamini wa Nasser kupitia Matoleo yake yote ya hapo awali ulikuwa unashughulikia kujadili masuala makuu zaidi ya Afrika kisha umetoa mapendekezo mengi ambayo yamerushiwa na wenye haki ya kukata uamuzi ndani yake.
Na Hassan Ghazaly, Mratibu mkuu wa Toleo la nne la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ameashiria mapokezi ya Wizara ya Vijana na Michezo jana na asubuhi ya leo kwa wajumbe washiriki wa Udhamini huo kutoka kwa ( Tanzania, Tunisia, Afrika Kusini, China, Azerbaijan, Brazil, Palestina, Sierra Leone, Urusi, Morocco, Oman, Jordani, Chad, Pakistan, Cameroon, Lebanon, Armenia, Niger, Mexico na Algeria)
Comments