Vijana wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa washiriki katika Marathoni kubwa zaidi ya Baiskeli katika mji mkuu mpya wa utawala
- 2023-06-07 10:56:09
Wajumbe Vijana wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la nne, Jumatano asubuhi, wameshiriki katika marathoni ya Baiskeli iliyoandaliwa na Wizara ya Vijana na Michezo ikisimamiwa na Dkt. Ashraf Sobhy katika Mji Mkuu Mpya wa Utawala katika kuadhimisha Siku ya Baiskeli Duniani, ambapo marathoni ilianza mbele ya jengo la Mamlaka ya Udhibiti wa Utawala, kuelekea wilaya ya serikali katika Mji Mkuu Mpya wa Utawala, kupita majengo ya mji mkuu.
Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, alisisitiza umuhimu wa kuandaa marathoni za Baiskeli katika Mji Mkuu Mpya wa Utawala ndani ya muktadha wa kuendana na maendeleo ya hivi karibuni ya kimataifa ili kuboresha mfumo wa kazi na vifaa vya utawala wa serikali, kwa kuzingatia maagizo na ujali wa Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri, kueneza michezo kote Jamhuri, kudumisha viwango vya afya ya umma na uzima wa mwili kwa wananchi wote, haswa Vijana, na kufanya michezo kuwa njia ya maisha ili kufikia moja ya malengo muhimu ya serikali katika uwanja wa michezo na afya, kwa kuhamasisha vijana Mazoezi, haswa Baiskeli.
Hassan Ghazali, Mratibu Mkuu wa toleo la nne la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, alisema kuwa wajumbe vijana wanaoshiriki katika Udhamini huo wa Nasser kutoka nchi (Tanzania, Tunisia, Afrika Kusini, China, Azerbaijan, Brazil, Palestina, Sierra Leone, Urusi, Morocco, Oman, Jordan, Chad, Pakistan, Cameroon, Lebanon, Armenia, Niger, Mexico, na Algeria) walishiriki katika marathoni kubwa zaidi ya Baiskeli kwa mahudhurio ya Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, na Meja Jenerali Khaled Abdel Aal, Gavana wa Kairo, aliyezindua ishara ya kuanza kwa marathon, na ushiriki wa washiriki zaidi ya 5,000 kutoka kwa mikoa mbalimbali.
Comments