"Miaka 60 tangu kuanzishwa kwa Jumuiya ya Nchi Huru za Afrika" Kikao cha mjadala cha kwanza cha Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la nne

Alhamisi, matukio ya toleo la nne la "Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa", unaofanyikwa kwa Ufadhili wa Rais Abdel Fattah El-Sisi - Rais wa Jamhuri, ilihitimishwa kwa kikao  cha mjadala cha kwanza kilichoitwa "Miaka 60 tangu uanzishaji wa Jumuiya ya Umoja ya Nchi Huru za Afrika", kwa mahudhurio ya Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, na kikundi cha viongozi wa Wizara ya Vijana na Michezo, Watengenezaji wa Vyombo vya habari na waandishi wa habari.

Kikao cha mjadala kilianzishwa na mtengenezaji wa vyombo vya habari, Mohamed Sayed Mahfouz, aliyesisitiza umuhimu wa kujenga mwamko wa kitaasisi kwa viongozi vijana, na umuhimu wa Jumuiya ya Umoja wa Afrika. Kikao hicho kilisimamiwa na Dkt. Noha Bakr, Profesa wa Sayansi za Siasa na mjumbe wa Baraza la Kitaifa la Haki za Binadamu, Balozi Nader Fath Al-Alim, Mwakilishi wa Umoja wa Afrika na mshauri mkuu wa kisiasa wa Umoja wa Afrika, na Yara Odah, Mjitolea wa zamani katika Umoja wa Afrika na mhitimu wa Mpango wa Kujitolea wa Umoja wa Afrika.

Kikao hicho kilijadili Ajenda ya 2063, changamoto na fursa zinazoikabili, na jinsi Umoja wa Afrika unavyoweza kujenga Amani na Usalama, pamoja na kuadhimisha miaka 60 ya maoni yaliyowekwa na waasisi wa Umoja wa Afrika, na kuwa bara hilo litakuwa kujengwa kwa hatua mpya huku kueneza ari ya amani Barani Afrika, kuhakikisha haki ya kijamii kwa mtu wa Afrika, kutumia rasilimali ili kujenga Bara la Afrika, na pia nafasi ya umoja katika kuunda na kuendeleza sera zilizopo, ili vijana wanaunda katika mawazo na ujenzi.

Mwanzoni mwa hotuba yake, Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, aliwakaribisha wajumbe wote wa vijana wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa katika toleo lake la nne, akieleza kuwa Udhamini huo ni moja ya programu muhimu za vijana ambazo daima huangaliwa na Mheshimiwa Rais Abdel Fattah El-Sisi - Rais wa Jamhuri, akiashiria umuhimu wa Falsafa ya kutofungamana kwa upande wowote na Ushirikiano wa Kusini-Kusini, kuendeleza matendo yao kutokana na changamoto hizi kuu, kuwasiliana kuelekea malengo na data, na kufanya juhudi nyingi ili kuibua shabaha nyingi zinazonufaisha jamii na nchi za Kiafrika.

Sobhy alieleza kuwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa umechukua jina la Marehemu kiongozi Gamal Abdel Nasser, ikizingatiwa kuwa yeye ni mmoja wa viongozi muhimu kwa watu wa nchi zinazoendelea (Afrika - Asia - Amerika ya Kusini) na mmoja wa mifano ya ya kipekee ya uongozi, kwani anachukuliwa kuwa kielelezo safi na kielelezo cha kisiasa na kihistoria cha dhana ya uongozi kwa upande wake kiongozi aliyetaka kuunga mkono harakati za ukombozi wa kimataifa hadi zikapata uhuru wao.

Mwanzoni mwa hotuba yake Balozi Nader Fateh Al-Alim, mwakilishi wa Umoja wa Afrika akisalimiana na Waziri wa Vijana na Michezo Dkt. Ashraf Sobhy, Viongozi waliohudhuria kutoka Wizara ya Vijana na Michezo pamoja na viongozi wa vijana walioshiriki katika toleo la nne la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, akiashiria kuwa bara la Afrika linawasubiri vijana wake wengi, na "Al-Alim" akaongeza kuwa tunasherehekea Mei 25, mwaka wa 2023 miaka 60 ya maono yaliyowekwa na mababa wanzilishi wa Umoja wa Afrika waliokuwa na maono makubwa na kazi yao kubwa ilikuwa ni kueneza ari ya amani Barani Afrika na kisha uadilifu wa kijamii kwa Mwafrika ili aweze kupanda katika madaraja ya maendeleo, na alisisitiza mnamo wa hotuba yake kuwa Ajenda ya Afrika ya 2063 ilizinduliwa kama maono na imetokana na ari ya mababa waasisi waliozungumzia umoja wa Afrika ulioendelea kutoka shirika hadi kuwa Umoja wa Afrika na haya si mabadiliko ya jina bali ni mabadiliko kwa ajili ya ya maendeleo na ili wajukuu waweze kukabiliana na changamoto zinazowakabili sasa, akiashiria kuwa ni maono yake ya tamaa isiyo na kikomo na upanuzi wa kweli wa maono ya mababa waanzilishi walioiweka Afrika kwenye njia sahihi.

"Mwakilishi wa Umoja wa Afrika" ameeleza kuwa Afrika baada ya Vita Baridi ilirithi idadi kubwa ya migogoro, na kuwa Mwafrika angeyeweza kuishi kwa chini ya dola moja aliweza kuishi na kupinga hali na changamoto zote, na alisisitiza kuwa Umoja wa Afrika hajawahi kuwatelekeza watu wa Kiafrika, na hakumuangusha mtu yeyote siku yoyote, na kuwa kuna maendeleo makubwa katika uwanja wa Amani na Usalama Barani Afrika kwa kuzingatia maslahi ya uhandisi wa Amani na Usalama, ambapo ilikuwa bidhaa wa maslahi ya amani na usalama barani Afrika ambayo Idara ya Amani na Usalama ilianzishwa, ambayo dhamira yake ni kushughulikia masuala ya migogoro, na kwa sababu hiyo, idara hiyo ilikuwa inaanzisha taratibu zinazomsaidia mtoa maamuzi kutekeleza maamuzi, na "Al- Alim" aliongeza kuwa watu wa bara la Afrika ndio wanaolinda amani na usalama barani Afrika, pia wanalinda maendeleo ya bara la Afrika, licha ya changamoto kubwa zinazopitia amani na usalama barani Afrika, lakini bado wanapigana hadi wapate amani na usalama Barani Afrika.

Yara Odah, Mjitolea wa zamani katika Umoja wa Afrika, alielezea furaha yake kwa kuwepo leo katika kikao hicho, kilichojumuisha matukio ya toleo la nne la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa. Alishukuru Wizara ya Vijana na Michezo na Ofisi ya Vijana wa Afrika kwa kumpa nafasi ya kuhudhuria leo, akionesha mwanzo wa kujitolea kwake katika Wizara ya Vijana na Michezo kupitia Ofisi ya Vijana ya Afrika, iliyokuwa kutoa msaada wote katika uwanja wa kuongeza mwamko kwa vijana kuhusu Afrika kupitia hatua nyingi ilizopitia tangu kujiunga na toleo la saba la Mpango wa Kujitolea wa Umoja wa Afrika uliofanyika nchini Misri mwaka wa 2016, na Odah alielezea changamoto alizokutana nazo na maendeleo, uboreshaji na tofauti zilizomkuta katika nchi za Afrika, ambapo alisafiri kwanza kwenda Ghana na kisha akajiunga na kufanya kazi katika Umoja wa Afrika, uzoefu huo ambao alishuhudia sana na kupitia huo alifanyia kazi ajenda ya vijana na kuwasilisha mapendekezo yote kwa vijana, na uzoefu mwingi alionao aliopitia na kufanya kazi na washirika wengi wa maendeleo, iliyomfanya ajifunze sana. Kisha akapata uzoefu mpya katika nchi tofauti aliposafiri kwenda Ethiopia, ambapo uzoefu wa kazi uko nyuma ya uzoefu wa kusoma au kusafiri kwa utalii, tunayopata mabadilishano makubwa ya kitamaduni na kukutana na watu kutoka nyanja na nchi mbalimbali, akibainisha kuwa kupitia Umoja wa Afrika amesafiri katika nchi kumi na tatu kuhudhuria makongamano, na amegundua kuwa vijana wana mchango mkubwa katika kuunda sera zilizopo na mkusanyiko wa uzoefu wa vijana ni kitu kitakachohakikisha malengo yaliyotarajiwa, na aliwahimiza vijana wote kusafiri na kugundua tamaduni mpya katika tukio ambalo kuna fursa yoyote kwao kusafiri na kuwa katika nchi mpya.
Washiriki wa "Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa" waliuliza maswali, maulizo na afua kadha baada ya wazungumzaji walimaliza hotuba zao katika kikao kilichofanyika mwishoni mwa matukio ya Alhamisi ya udhamini huo. Kisha washiriki wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa walipiga picha za ukumbusho huku kukiwa na mwingiliano, shangwe na furaha kutoka kwa kila mtu aliye na kipindi hiki mashuhuri na habari muhimu waliyopata.

Comments