Maelezo juu ya Mwenendo wa Baba Waanzilishi wa Harakati ya kutofungamana kwa Upande Wowote" kwenye kikao cha majadiliano la toleo la nne la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa
- 2023-06-07 11:04:16
Leo, Ijumaa, mnamo Juni 2, shughuli za Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa , zimezinduliwa katika toleo lake la nne, kikao mazungumzo chake cha kwanza kwa kichwa cha habari "Maelezo juu ya Baba Waanzilishi wa Harakati ya kutofungamana kwa Upande wowote" kwa mahudhurio ya Mr.Hassan Ghazali, Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa na kundi la viongozi wa Wizara ya Vijana na Michezo na watangazaji na waandishi wa habari.
Kikao hicho kilihudhuriwa na Eng.Abdel Hakim Gamal Abdel Nasser, Mwana wa marehemu kiongozi Gamal Abdel Nasser, Balozi Miroslav Cestovic Balozi wa Serbia, Balozi Lutfi Raouf Balozi wa Indonesia, na Hajj Muhammad Alijah, Mwanzilishi wa Benki ya Chakula nchini Ghana na kiliongozwa na mtangazaji Samy Aisawy ambaye mwanzoni, alizungumzia Kuanzishwa kwa Harakati ya Kutofungamana kwa upande wowote na Waanzilishi wake.
Pamoja na falsafa yake, pia alishughulikia migogoro inayoendelea na jinsi tunavyoweza kukabiliana nayo mnamo siku zijazo, akielezea kuwa watu hawakuwa na motisha kwa hivyo , hawakuweza kufanya chochote kuhusu maisha yao ya baadaye, na alisisitiza umuhimu wa wa kujua historia ili tujue mizizi, njia na maelekezo sahihi kwa mustakabali .
Mhandisi Abdel Hakim Gamal Abdel Nasser, Mwana wa marehemu kiongozi Gamal Abdel Nasser, mwanzoni mwa hotuba yake alitoa salamu kwa viongozi vijana walioshiriki katika uzinduzi wa nne kwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa , akielezea furaha yake kwa kuzungumzia mada inayotugusa sote hivi karibuni, haswa wakati wa hali ya sasa anayopitia ulimwenguni kote na akiongeza kusema kuwa Harakati ya Nchi Zisizofungamane kwa Upande Wowote ni kama mwana halali aliyekuja baada ya ukombozi kutoka kwa ukoloni na kurudisha kwa utashi wa Rais wao baada ya watu hao kutawaliwa na ukoloni wakati wa karne ya 19 na mwanzo wa karne ya 20, ambapo wakati huo haikukubalika kwa nchi yoyote kupata Uhuru wake wakati wa kuwepo madaraka makubwa na yanazitawala nchi hizo, na mwana wa marehemu kiongozi, Gamal Abdel Nasser, alionesha wakati wa hotuba yake jukumu la marehemu kiongozi, Gamal Abdel Nasser, katika kuanzisha Harakati ya Nchi Zisizofungamana kwa upande wowote, mikutano na safari zake kadha, mahusiano yake na viongozi wa nchi na yale waliyoyakubali katika Harakati ya Kufungamana kwa upande wowote, na mawazo yake juu ya kupambana na ukoloni na kukataa kwake kwa wazo au makubaliano yoyote yenye maslahi kwa madola makubwa dhidi ya maslahi ya nchi zinazoendelea, ambapo alitambua kuwa isitokuwa na uwiano, yatapowepo madola makubwa zinazozingatia maslahi yao dhidi ya maslahi ya nchi zinazoendelea .
Mwanzoni mwa hotuba yake, Balozi Miroslav Cestovic, Balozi wa Serbia, alitoa shukrani zake kwa Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, kwa mwaliko wa kuhudhuria kikao cha mazungumzo hicho , na kwa kuandaa Udhamini wa Nasser wa Uongozi wa Kimataifa ; Udhamini huo ulio muhimu, hasa kwa wakati wa hitaji la ulimwengu la uongozi wa vijana mnamo kipindi cha hivi sasa , ikionesha kwamba Historia imetoa mifano kwa marais na viongozi katika nyakati nyeti katika zama zote.Miroslav, katika hotuba yake, alizungumzia historia ya kuanzisha kwa harakati ya Nchi Zisizofungamane na Siasa za Upande Wowote, akieleza kuwa mnamo kipindi cha zaidi ya miaka 60 tangu mkutano wa kwanza wa kilele wa harakati ya Nchi Zisizofungamana kwa upande wowote tunaona kwamba ulimwengu unabahatika kwamba harakati hiyo kuwa Mpango wa viongozi watano uliopata sifa ya kipekee ya kimataifa wakati huo , na nchi nyingi za Ulaya zilijiunga nayo.Pengine wakati huo walikuwepo wale walioshangaa kwamba inapatikana nchi za Ulaya zilizojiunga katika Harakati hiyo.Balozi wa Serbia alizungumzia sherehe hiyo iliyoandaliwa katika maadhimisho ya miaka 60 ya Harakati ya kutofungamana kwa Upande Wowote, akisisitiza kwamba roho na falsafa ambayo harakati hiyo iliitegemea wakati wa kuundwa kwake ,bado ipo hadi sasa, na kwamba kutokana na urithi ambao harakati hiyo iliutuachia ,tutakalolifanya linatutegemea sisi pamoja na vijana ambao ni viongozi wa mustakabali.
Kwa hiyo, ni muhimu kuwa na maono wazi na imara ili kukabiliana na changamoto kama vile, zilikuwepo kabla ya kuanzishwa kwa harakati isiyofungamana kwa upande wowote.
Balozi Lutfi Raouf, Balozi wa Indonesia, mwanzoni mwa hotuba yake katika kikao cha mazungumzo, alisisitiza kuwa amefurahishwa na kujivunia kuwa miongoni mwa hadhira waheshimiwa na viongozi vijana wanaoshiriki katika Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa, na kurejesha kumbukumbu na historia ya kiongozi Gamal Abdel Nasser, vilevile, katika hotuba yake aligusia kuanzishwa kwa harakati ya kutofungamane kwa upande wowote. pia alionesha video inayofafanua msimamo uliofuatiliwa na kiongozi Gamal Abdel Nasser na ndoto na matumaini yanayohusiana na harakati ya Nchi Zisizofungamana kwa Siasa za Upande Wowote, akiashiria kuwa mkutano wa nchi za Asia mwaka 1955 ulikuwa mkutano muhimu sana ambapo kanuni za Usawa kati ya nchi zote na raia , amani kutoka kwa migogoro yoyote kwa wakati huu, na kutotumia silaha au ukatili, hasa lilihusiana na maslahi yoyote ya binafsi kwa chama chochote , zilikubaliwa ambazo baadaye zimekuwa ndizo ni mawazo na kanuni ambazo Harakati ya Nchi Zisizofungamana kwa upande wowote ilizitegemea kisha mikutano ilifuata hadi imeainishwa Ajenda na malengo , Balozi wa Indonesia, alionesha hatua tofauti za kuzindua kwa Harakati isiyofungamana kwa upande wowote, akisisitiza kwamba miongoni mwa mambo muhimu kwa vijana ni kujua mtiririko wa harakati hiyo isiyofungamana kwa upande wowote, ambapo walishirikisha katika kuanzishwa kwake wanachama wapatao 25 hadi imefikia wanachama wapatao 120 pamoja na nchi 19 zinazofuatilia harakati hiyo. kwa na wakati tunayashuhudia kutoka kwa machangamoto mengi yakiwemo hali ya kiuchumi, majanga ya ndani na asilia yanayotokea katika nchi kadhaa na mengineyo , kwa hivyo tunahitaji sasa baadhi ya mawazo yanayoweza kutusaidia katika baadhi ya matukio, hivyo kanuni za harakati isiyofungamane na upande wowote yenye umuhimu mkubwa ambazo ndizo zitakazochangia katika kutafuta suluhu na kuunganisha umati na sauti . pamoja na kuunda na kufikia masuluhisho kwa matatizo hayo kwa njia tofauti isiyo ya kawaida na kutoa mapendekezo ya kushinda machangamoto haya, na kufanya kazi ya kuunganisha umati ya nchi zilizoshiriki katika harakati hiyo ili kupata amani na uhuru, na alitoa ushauri wake mwishoni mwa hotuba yake kwa vijana wasomi wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi , kwamba kutosahau historia kwa sababu ni ndiyo inayoainisha njia yetu na kupitia kwa kujua historia, tunaweza kuunganisha yaliyopita na ya sasa kwa ajili ya kuifanya nchi yetu kuwa imara.
Alhaji Muhammad Alijah, Mwanzilishi wa Benki ya Chakula nchini Ghana, alieleza furaha yake yakuwepo baina ya viongozi vijana walioshiriki katika toleo la nne la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa , akiashiria kwamba Harakati isiyofungamana kwa upande wowote ni harakati muhimu sana, na kwamba kuna daima swali linalomjia kichwani inayohusiana na kanuni au misingi ambayo ilifanikiwa kwa Mpango wa Tano au ule unaoitwa Mpango usiofungamane kwa upande wowote, ambao inawezekana kwa kusoma vitabu vya kijamii , kujibu kwa misingi ile ilikuwa mitatu. : amani, mshikamano na uhuru, kwa hivyo tunakuta wakati huo , nchi zilikuwa zikitetea harakati ya Nchi Zisizofungamana kwa upande wowote kutoka moyoni, hivyo basi nchi zote hizo zikiwa za Mashariki au Magharibi zinatetea haki yake ya uhuru na kuwa nchi zinazojitawala binafsi. Kwa njia hii, mshikamano uliwawezesha raia wote kuamua kuwa wanajihusisha na upande gani, Mashariki au Magharibi, kwa kuendelea utambulisho wao wenyewe, na kauli mbiu ya Amani inapambanua ambayo ulimwengu uliihitaji wakati huo, na mwanzilishi wa benki la chakula la Chama alisisitiza kwamba kila mtu anajihusisha kwa harakati isiyofungamane na Upande Wowote na kwamba sote tunapaswa kupenda raia wetu na kutambua kwamba raia hawa tu ndio wana haki ya kuamua hatima yao wenyewe na kuishi kwa amani, uhuru na mshikamano. na Alijah alitaja mifano ya viongozi waliopigania uhuru ambaye Miongoni mwao ni kiongozi Gamal Abdel Nasser, ambaye alitaifisha mfereji wa Suez ili kuwahudumia wananchi wa Misri, kwani ni kwa Misri, na kila raia Mmisri anajivunia kwake kama ni sehemu kutoka kwao kwa hivyo inahusiana nao ,watu wa Misri, na kiongozi wa Ghana Kwame Nkrumah, ambaye alikuwa na jukumu kubwa katika uhuru wa Ghana, kwa kuwa alikuwa na taasisi nyingi alizianzisha nchi kadhaa, na katika mifano hiyo inaonekana wazi jinsi watu wanawapenda wale wanaowapenda na kutetea uhuru wao na raia wao, basi hapa uhuru ndio ni njia ya kutekeleza hivyo.
Idadi ya washiriki walioshiriki kwa kuuliza maswali, na maongezi - baada ya wasemaji walimaliza hotuba zao -katika kikao kilichofanyika mwanzoni mwa shughuli siku ya Ijumaa asubuhi na kutoka kwa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ambacho kulizungumzia njia ya waanzilishi wa Harakati ya kutofungamana kwa upande wowote, kisha washiriki wa Udhamini huo walipiga picha za kumbukumbu wakati kukiwa na mawasiliano, shangwe na furaha na kila mtu kwa kikao hiki kinapambanua na habari zilizo muhimu walizipata.
Kwa upande wake, Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa , Hassan Ghazali alieleza kuwa katika toleo la nne la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa wanashiriki viongozi vijana kutoka nchi za Tanzania, Tunisia, Afrika Kusini, China, Azerbaijan, Brazil, Palestina, Sierra Leone, Russia, Morocco, Oman , Jordan, Chad, Pakistan, Cameroon, Lebanon, Armenia, Niger, Mexico, na Algeria) ambapo walishiriki jana, Jumatano, katika mbio za baiskeli zilizoandaliwa na Wizara ya Vijana na Michezo katika Mji Mkuu Mpya wa Utawala ikiwa miongoni mwa sherehe za siku ya baiskeli ya ulimwenguni . vilevile , Shughuli za jana zilijumuisha kikao cha kufahamiana kati ya washiriki wa Udhamini huo kutoka nchi mbalimbali.
Ikumbukwe kwamba Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ni mojawapo ya mifumo ya utendaji ili kutekeleza mapendekezo ya Rais Abdel Fattah El-Sisi - Rais wa Jamhuri, kwa lengo la kuunga mkono kwa vijana hodari wa Kiafrika, kuwawezesha kuunda maoni ya kina na muhimu yanayohusishwa na masuala ya kimataifa na mipango ya maendeleo endelevu, na pia kuunga mkono fursa za kutangaza jukumu la Misri ulimwenguni kote kama inavyokuja ndani ya mfumo wa kutekeleza maono ya Misri kwa malengo ya Maendeleo Endelevu 2030, Ajenda ya Afrika 2063, na Ushirikiano wa Kusini-Kusini.
Comments