"Njia mbadala za kiuchumi za kusini mwa Dunia" miongoni mwa Mazungumzo ya Toleo la Nne la Udhamini wa Nasser kwa mahudhurio ya Balozi wa Singapore
- 2023-06-07 11:10:53
Shughuli za jioni ya siku ya tatu ya" Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa" katika toleo lake la nne zilihitimishwa kwa kikao cha majadiliano chenye kichwa “ Njia Mbadala za Kiuchumi za Kusini mwa Dunia" kwa ushiriki wa Balozi Dominic Goh, Balozi wa Singapore nchini Misri, Dkt. Samuel Egba, Mtafiti katika Kituo cha Usuluhishi Barani Afrika katika Chuo Kikuu cha Pretoria, Giuliana Seledonio Digani, Mkurugenzi Mkuu wa Kamisheni ya Ulaya ya Ushirikiano wa Kimataifa.na kikao hicho kilisimamiwa na Ravello Prigo.
Kwa upande wake, Mratibu Mkuu wa Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa , "Hassan Ghazali" alieleza kuwa Viongozi mashuhuri Vijana wakishiriki katika toleo la nne la Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa kutoka nchi za ( Tanzania, Tunisia, Afrika Kusini, China, Azerbaijan, Brazil, Palestina, Sierraleone, Russia, Morocco, Oman, Jordan, Chad, Pakistan, Cameroon, Lebanon, Armenia, Niger, Mexico, na Algeria) na wameshiriki jana Jumatano katika Marathon ya Baiskeli iliyoandaliwa na Wizara ya Vijana na Michezo katika mji Mkuu mpya wa utawala miongoni mwa sherehe za Siku ya Baiskeli Duniani, shughuli za jana zilijumuisha kikao cha utambulisho baina ya washiriki wa Udhamini kutoka nchi mbalimbali.
Mratibu Mkuu huyo wa Udhamini huo aliongeza kuwa warsha zilifanyika wakati wa shughuli za jana, Jumamosi, Wajumbe wa Udhamini huo wenye uwezo maalum walishiriki katika hilo -kwa mara ya kwanza - ambapo majadiliano yalifanyika kuhusu jinsi ya kuwaunganisha watu wenye uwezo maalum katika taasisi za kazi, na warsha zilishughulikia changamoto ambazo watu wenye ulemavu wanakabiliana nazo katika taasisi mbalimbali za kazi ndani ya nchi mbalimbali, pamoja na kuzungumzia jukumu la serikali, jukumu la kiraia. jamii, na jukumu la taasisi za kazi zenyewe katika kuunganisho huo, Washiriki pia wakaonesha kundi la mapendekezo yatayopitishwa na Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kimataifa katika toleo lake la nne.
Ikumbukwe kwamba Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa Kimataifa ni mojawapo ya mifumo ya utendaji ya kutekeleza mapendekezo ya Rais Abdel Fattah El-Sisi, Rais wa Jamhuri;kusaidia Vijana waafrika,na kuwawezesha kuunda maoni ya kina na muhimu yanayohusishwa na masuala ya kimataifa na mipango ya Maendeleo Endelevu, na kuunga mkono fursa za kukuza jukumu la Misri Duniani kote kwani inakuja miongoni mwa mfumo wa utekelezaji wa maoni ya Misri ya Malengo ya Maendeleo Endelevu ya 2030, Ajenda ya Afrika 2063, na Ushirikiano wa Kusini-Kusini.
Comments