Waziri wa Michezo kwa Wachezaji wa Timu ya Olimpiki kwenye Uwanja wa Ndege wa Kairo" Nyinyi ni Mashujaa"

Jumatatu asubuhi Julai 10, Dkt. Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo aliwapokea ujumbe wa timu yetu ya Olimpiki baada ya kurudi kutoka Morocco, na kupata nafasi ya pili na medali ya fedha katika Kombe la Mataifa ya Afrika chini ya miaka 23 na kufuzu kwa Michezo ya Olimpiki ya Paris 2024.

Dkt. Ashraf Sobhy alisema katika ujumbe wake kwa wachezaji wa timu hiyo:

" Leo tunakupokeni kama mabingwa, hukupungukiwa na kufanya kile unachohitaji, asanteni, na tungoje kwenu Paris na kutoa onesho linaloiheshimu nchi ya Misri, isiyopungua juhudi katika kutunza michezo na wachezaji, tunasubiri timu yetu ya Olimpiki katika Olimpiki ya Paris ili kupata utendaji uliyo bora zaidi na kufikia nafasi za juu, sio uwakilishi wa heshima."

Waziri akaendelea: "Ninawajivunia nyinyi kwa kiwango cha mbali zaidi, mlionesha utendaji bora kweli na uungwana, mliiheshimu Misri na kutuheshimu sisi sote. Jana tulikuwa kwenye mkutano na waandishi wa habari kwa Ligi ya Misri katika Mji Mkuu Mpya wa Utawala, ilionesha nguvu ya Misri.”

Dkt. Ashraf Sobhy aliwashukuru na kuwathamini wafanyakazi wa ufundi wa timu ya taifa wakiongozwa na Mikali ambaye aliwashughulikia wachezaji wa timu hiyo kwa weledi na upendo mkubwa na kuwafikisha katika kiwango cha kupambana walichoonesha wakati wa mechi za mashindano hayo, hasa, timu ya taifa ilicheza kasoro ya mchezaji dhidi ya timu ya taifa ya Morocco katika mechi ya fainali iliyofanyika huko Morocco.

Waziri wa Vijana na Michezo aliahidi kutoa njia zote za kusaidia timu za Misri katika ngazi za vifaa na maadili, katika mashindano mbalimbali yajayo na kwa muda mrefu pia, kwa ushirikiano na uratibu na mashirikisho ya michezo na taasisi za kiraia na sekta binafsi.

Waziri huyo aliashiria kuwa maagizo ya Rais Abdel Fattah El-Sisi, na uungaji mkono wake endelevu na ufuatiliaji wa faili ya kazi katika mfumo wa vijana na michezo, Misri imewekwa katika nafasi isiyo ya kawaida, akibainisha kuwa mipango ya kisayansi na mkakati kulingana na kazi inayofanywa na timu za kitaifa, pamoja na kutoa njia zote za msaada kwao, michezo ya Misri imekuwa ikisonga kwa kasi kubwa kuelekea kufikia mafanikio makubwa.

Comments