Waziri wa Michezo, Gavana wa Aleksandria na Rais wa shirikisho la kiafrika wanashuhudia mechi ya ufunguzi wa kundi la pili katika uwanja wa Aleskandria.

Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, Dokta. Abdelaziz Kansoua gavana  wa Aleksandria, na Ahmed Ahmed, rais wa Shirikisho la Soka la kiafrika, walitazama  mechi ya ufunguzi wa kundi la pili kati ya Nigeria na Burundi, ambayo ilimalizika kwa ushindi wa Nigeria kwa goli moja bila ya lolote.

 

Waziri wa Vijana na Michezo aliusifu  uzuri wa uandaaji ,  uliotokeza picha chanya  kwa  timu zilizoshiriki na wajumbe waliokuwa wakiambatana  nao.

 

Na mnamo  mechi, Dokta. Ashraf Sobhy,  Waziri wa Vijana na Michezo, na Dokta. Abdelaziz Kanswa, Gavana wa Aleskandria, walimpa kitabu cha Misri kama zawadi  kwa Ahmed Ahmed, Rais wa Shirikisho la Soka la kiafrika, kilichokusanya historia ya Misri, na kilichoandaliwa na maktaba ya Aleksandria .

 

Mechi ilihudhuriwa na Hani Aburida, rais wa Shirikisho la Soka la kimisri, Mohamed Fadl, mkurugenzi wa michuano , na nyota wa soka la kiafrika Samuel Sto'o, walikuwa wajumbe wa Shirikisho la Soka la kiafrika.

 

Inatajwa kwamba uwanja  wa Aleskandria unakaribisha kundi la  pili linalojumisha timu za  Nigeria, Guinea, Burundi, Madagascar,

Katika mashindano ya Kombe la Mataifa ya kiafrika n. 32, ambayo  matukiuo  yake yalianza  jana na yataendelea mpaka Julai 19.

 

Comments