Kwa mahudhurio ya Mabalozi wanne toka nchi za kiafrika "Vijana na michezo" inahitimisha matukio ya "Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kiafrika " na inasherehekea kuwahitimu vijana wa kundi la kwanza.
- 2019-06-23 15:35:32
Leo, Wizara ya vijana na michezo kwa Uongozi wa Dokta Ashraf
Sobhy imehitimisha matukio ya Udhamini wa "Nasser kwa Uongozi wa
kiafrika"uliotolewa kwa Wizara (Ofisi ya vijana waafrika, na Idara kuu kwa
Bunge na Elimu ya kiraia) chini ya uangalifu wa Dokta Mustafa Madbuly
"Waziri mkuu"mnamo kipindi cha 8 hadi 22 Juni 2019 kwa kushirikiana
na Shirikisho la vijana waafrika.
Na sherehe ya kuwahitimu vijana wa kundi la kwanza toka Udhamini
wa "Nasser kwa Uongozi wa kiafrika " ilihudhuriwa na idadi kadhaa ya
mabalozi wa nchi za kiafrika, miongoni mwao ni Balozi wa Ruwanda, Balozi wa
Kongo , Balozi wa Zambia, Balozi wa Ethiopia, pamoja na Rais wa ofisi ya
Shirikisho la kiafrika kwenye Jamhuri ya Misri ya kiarabu Balozi "Abd
Elhamid Buzaher", Mwakilishi wa vijana waafrika Bwana "Monzer
Elmseraf", Bibi Dina Fouad "Rais wa Idara kuu kwa Bunge na Elimu ya
kiraia ", na Bwana Hassan Ghazali "Naibu wa Rais wa Shirikisho la
kiafrika, na Mwanzishi wa Ofisi ya vijana waafrika kwenye Wizara ya vijana na
michezo", na makada kadhaa wa Wizara.
Na mnamo kauli yake Bwana Monzer "Mwakilishi wa
Shirikisho la vijana waafrika " alisisitiza juu ya umuhimu wa Udhamini wa
"Nasser kwa Uongozi wa vijana waafrika" unaochangia kuwawezesha na
kuwaboresha vijana wa nchi za kiafrika kwa ajili ya kuhakikisha malengo ya
Shirikisho la kiafrika, kuunda, na kuendeleza Bara la kiafrika, akisifu mchango
na juhudi za uongozi wa kimisri kwa urais wa Abd Elfatah Elsisi ili kuunga
mkono vijana waafrika na kuchangia kuendeleza wananchi wa nchi za kiafrika
kupitia kuhamisha jaribio la Baba waanzishi wa Umoja wa kiafrika na khasa
Kiongozi aliyekufaGamal Abd Elnasser.
Na Bwana Elmesref alieleza mchango wa Misri na Kiongozi
aliyekufa Gamal Abd Elnasser katika kusaidia bara la kiafrika kupitia harakati
za Ukombozi zilizochangia Umoja wa Afrika mnamo zama zote, akisisitiza kwamba
vijana waafrika wana jukumu la kuboresha na kuunda bara la kiafrika pia
kutekleza Ajenda ya 2063 kwa ajili ya maendeleo, kuhakikisha utulivu, uhuru, na
ustawi kwa bara la kiafrika, pia aliahidi kwa kuendelea kuwasiliana pamoja na
vijana wa nchi za kiafrika ukiongezeka na kuimarisha Ushirikiano kati ya
Shirikisho na vijana waafrika kwa ajili ya kuunda uwezo wao ili kuwawezesha
kuongoza bara la kiafrika.
Na kwa upande wake Balozi Abd Elhamid Buzaher "Rais wa
ofisi ya Shirikisho la kiafrika kwenye Jamhuri ya Misri ya kiarabu "
alielezea furaha yake kubwa kwa kuwahitimu kundi la kwanza toka Udahmini wa
"Nasser kwa Uongozi wa kiafrika "uliotolewa kwa Wizara ya vijana na
michezo (Ofisi ya vijana waafrika, na Idara kuu kwa Bunge na Elimu ya kiarabu)
chini ya uangalifu wa Dokta Mustafa Madbuly "Waziri mkuu ",
akiashiria kwa Udhamini unachangia kubakisha kumbukumbu ya kiustarabu na
kisiasa kwa waafrika wote nayo ni kumbukumbu ya Kiongozi aliyekufa Gamal Abd
Elnasser aliyeanzisha Umoja wa bara la kiafrika.
Pia Balozi Buzaher alisifu dhana ya Udhamini iliyochaguliwa
kwa Wizara ya vijana na michezo, kulingana na Imani ya uongozi wa kimisri kwa
umuhimu wa kuhamisha jaribio la shughuli ya kiraia na mitazamo ya kimikakati na
kisiasa zilizotumiwa na Kiongozi aliyefariki Gamal Abd Elnasser kwa vijana
waafrika kwa ajili ya kupata faida toka historia ya mapambano yake kupitia harakati
za Ukombozi na kuthibitisha dhana ya kweli kwa uhuru na utulivu, pamoja na
kutoa mwanga wa mchango wa Baba waanzishi wa Umoja wa kiafrika, akisisitiza juu
ya dharura ya kueneza uwiano wa kisiasa, kueneza dhana ya uhuru na kuzingatia
Elimu na kuwezesha pamoja na kuongeza juhudi na kuimarisha Ushirikiano kati ya
nchi za kiafrika kwa ajili ya kuunda uwezo wa vijana waafrika kuwazingatia
mustakbali ya bara na wahusika wa uteklezaji wa Ajenda 2063 na kuliongoza
Afrika.
Na wakati huu huu Profesa Elsayd Flefil "Rais wa kamati
ya masuala ya kiafrika kwenye Bunge, na Mkuu mkale wa Kitivo cha masomo ya juu
ya kiafrika" alisisitiza kwamba Udhamini wa Nasser kwa Uongozi wa kiafrika
ulichangia kuhamisha jaribio la kimisri kwa nchi za kiafrika kwa lengo la
kuhakikisha maendeleo na uteklezaji wa Ajenda ya 2063,akiwaita vijana washiriki
katika Udhamini kwa kuhamisha ujumbe wa Upendo kwa nchi zao za kiafrika toka
Shirikisho la kiafrika kulizingatia Mwavuli unaojumuisha waafrika na Nyumba
ambayo pande zake hujengwa na nchi za kiafrika.
Pia aliwaomba vijana waafrika kukamilisha mwelekeo wa Baba
waanzishi wa Umoja wa kiafrika, na kuibeba jukumu la kujenga Afrika ya pekee,
lenye Sauti moja kwa ajili ya kwa kufikia 2063 tutatatua masuala na matatizo
yote ya bara la kiafrika, akiomba kwa dharura ya kufahamu aya zote za Ajenda
2063 kwa upendo ili kuzitekleza kwa kweli kwa ajili ya kumaliza Maradhi,
Ujinga, Umaskini, Kuzingatia Elimu, na kuwezesha ili kujenga mustakbali ya bara
la kiafrika kwa juhudi za wana wake, akisisitiza juu ya dharura ya maendeleo ya
kuwasiliana kati ya nchi ili kubadilishana na kuhamisha uzoefu kati ya nchi za
kiafrika, na umuhimu wa kuwaelimisha vijana waafrika kwa ujumbe wa Kiongozi
aliyefariki Gamal Abd Elnasser katika nyanja zote ili kujenga bara kwa vizazi
vitakavyokuja.
Na kutoka upande wake Bibi Dina Fuad "Rais wa Idara kuu
kwa Bunge na Elimu ya kiraia " alisisitiza kwamba Udhamini wa Nasser wa
Uongozi wa kiafrika ambapo hushiriki ndani yake vijana 100 wanaowakilisha nchi
25 za kiafrika, unakuja katika mfululizo wa Programu na matukio yanayopangwa
kwa Wizara ya vijana na michezo kwa Uongozi wa Dokta Ashraf Sobhy, kwa lengo la
kuimarisha mchango wa vijana waafrika kupitia kutoa njia zote za usaidizi na
uwezeshaji pamoja na kuwawezesha katika vyeo vya kuongoza na kupata faida toka
uwezo na mawazo yao, kutekleza kwa yaliyotangazwa na Rais wa Jamhuri mnamo
matukio ya mkutano wa vijana wa dunia.
Wakati ambapo Bwana Hassan Ghazali "Naibu wa Rais wa
Shirikisho la kiafrika, na Mwanzishi wa Ofisi ya vijana waafrika kwenye Wizara
ya vijana na michezo" alisisitiza kwamba Udhamini wa "Nasser kwa
Uongozi wa kiafrika "unazingatiwa kipengele kimoja cha vyanzo vya
kuwezesha kwa ugeuzi wa kiafrika vilivyoidhinishwa kwa Ajenda ya Afrika 2063,
na kimoja cha kutekleza mpango wa (1Million by 2021) ili kuwawezesha vijana
waafrika milioni moja kwa kufikia mwaka wa 2021 uliotolewa kwa Kameshina ya
Sayansi, Teknolojia, na Rasilimali za binadamu katika Umoja wa kiafrika,
akifafanua malengo yake yanayowakilishwa katika kuhamisha jaribio kale la kimisri
katika kuunda taasisi za kitaifa, na kuunda kizazi kipya cha makada waafrika
vijana wa kimageuzi wenye mitazamo inayosawazisha na mielekeo ya urais wa Misri
kwa Umoja wa kiafrika yenye Imani ya kuhudumia malengo ya Umoja wa kiafrika
kupitia Ukamilifu, pamoja na kuunda mkusanyiko wa makada waafrika vijana wenye
athari kubwa barani kwa kufunza,uzoefu unaolazimishwa, na mitazamo ya
kimikakati.
Na matukio ya Hitimisho yalijumuisha kauli ya Aya Sheby
"Mjumbe wa vijana wa Shirikisho la kiafrika " kupitia Rikodi
inayobeba ujumbe wa upendo kwa vijana waafrika washiriki katika matukio ya
Udhamini wa "Nasser kwa Uongozi wa kiafrika", akiashiria kwa mchango
wa Misri na Wizara ya vijana na michezo katika kuwafundisha na kuwawezesha
vijana waafrika kwa Uongozi na kujenga na kuendeleza bara, baada yake kifungu
cha ushauri kwa inwani ya "SISI" kilichotolewa na mshiriki mmoja wa
washiriki wa Udhamini toka nchi ya Uganda, na kifungu cha wimbo kinachoakisi
roho ya Afrika kwa idadi kadhaa ya washiriki na kwa Uongozi wa Ahmed Omar
"Mwanachama wa Timu ya West Elbalad", na sherehe ilihitimu kwa
kuheshima washiriki na kutoa vyeti vya kundi la kwanza toka Udhamini wa
"Nasser kwa Uongozi wa kiafrika".
Comments