Waziri wa Michezo anampokea rais wa Mauritania katika uwanja wa Suez.

Dokta Ashraf Sobhy, Waziri wa Vijana na Michezo, na Jenerali Abdul Majid Saqr Gavana wa Suez waliwapokea Rais Mohamed Ould Abdel Aziz wa Raisi wa Jamhuri ya Mauritania ya Kiislamu, na Bwana  Aruna Modibo Toure, Waziri wa Vijana na Michezo katika Nchi ya Mali kwenye uwanja wa Suez, ili kutazama mechi ya timu ya Mali dhidi ya timu ya Mauritania katika mzunguko wa kwanza wa Kundi la tano katika Kombe la Mataifa ya kiafrika No. 32.

 

Waziri wa Vijana na Michezo Dokta Ashraf Sobhy alimkaribisha Rais Mohamed Ould Abdel Aziz, Rais wa Jamhuri ya Mauritania ya Kiislamu, ambaye alikuja kwa ajili ya  kusimama pamoja na timu ya nchi yake Mauritania inayoshiriki katika Kombe la Mataifa ya kiafrika kwa mara ya kwanza na Waziri wa Vijana na Michezo ya Jamhuri ya Mali kusimama pamoja na timu ya nchi yake wakati wa michuano.

 

Rais wa Mauritania alisifu kukaribisha  Misri kwa michuano hiyo,pia  alisifu juhudi zilizofanywa na serikali ya kimisri katika maandalizi ya kukaribisha mashindano hayo wakati mdogo,  Rais wa Mauritania alieleza kushangaza kwake  kutoka sherehe ya ufunguzi wa michuano hiyo.

 

Waziri wa Vijana na Michezo alifuatilia maandalizi ya kundi la tano, ambayo lnakaribishwa kwa Uwanja wa Suez hadi wakati wa mwisho kabla ya kuanza kwa mechi ya Tunisia na Angola, ambayo ilimalizika na matokeo  chanya kwa 1/1.

 

Waziri wa Vijana na Michezo alikuwa na hamu ya kuhudhuria mechi za ufunguzi kwa  makundi yote ya Kombe la Mataifa ya kiafrika ili kufuatilia maandalizi ya mwisho ya viwanja na kuangalia juu ya shirika lenye manufaa.

Comments