Uwanja wa
Ismailia ni uwanja wenye matumizi kadhaa. Upo mjini Ismailia nchini Misri.
Uwanja huo ulikuwa miongoni mwa nyanja 6 zilizotumiwa katika Afcon (kombe la
mataifa la kiafrika) mwaka 2006 nchini Misri. Pia mechi kadhaa za kombe la
dunia kwa vijana mwaka 2009 nchini Misri zilichezwa katika uwanja huo. Uwanja
huo una uwezo wa kuchukua watazamaji 18.525. Uwanja huo unajumuisha: viwanja
viwili vya tennis,beseni, na gereji ya magari 15 takriban na idadi hii ni ndogo
kwa sababu ya kuwa uwanja huo upo mjini na watazamaji huweza kuufikia kwa
miguu. Kazi za kujenga uwanja huo zilianza mwaka 1934 lakini ulifunguliwa rasmi
mwaka 1947. Ardhi
ya uwanja huo ni nyasi asilia. Uwanja huo ni uwanja rasmi wa klabu vya Ismaili.
Comments