Uangalizi wa kuunda Ofisi ya kiutendaji kwa Mawaziri waafrika wa vijana na michezo.

Kwenye makao makuu ya Wizara, Waziri wa vijana na michezo Dokta Ashraf Sobhy aliwakutana pamoja na idadi kadhaa ya mawaziri wa vijana na michezo, na mabalozi wa nchi za kiafrika zinazoshiriki katika mashindano ya michuano ya kombe la mataifa ya kiafrika kwa Soka nchini Misri 2019 toka nchi za Morocco, Cameroon, Kenya, Senghal, Zimbabwe Cote d'lovoire, Algeria, Benin, Burundi, Congo, na Uganda.

 

Wakati wa mazungumzo yao mawaziri waheshemiwa hawa waliishukuru nchi ya kimisri kwa kupokea kuzuri kwake na uundaji bora kwa michuano ya kombe la mataifa ya kiafrika nchini Misri, khasa katika sherehe ya ufunguzi wa michuano juzi, pamoja na maendeleo bora kwa majengo na ufanisi wa viwanja vinavyokaribisha michuano, na heshima ya kukaribisha na kupokeza wa kimisri kwa wajumbe wote wa kiafrika wanaoshiriki katika michuano ya mataifa ya kiafrika.

 

Na mnamo kauli yake Sobhy alisisitiza juu ya dharura ya kuongeza ushirikiano na kuwasiliana kati ya nchi za bara la kiafrika, na alishauri kuunda ofisi ya kiutendaji kwa Mawaziri waafrika wa vijana na michezo inayohusiana na umoja wa kiafrika ili kuwa chombo kikuu kinachojumuisha nchi za bara na kiwe kama mwavuli wa Ushirikiano wa pamoja na kutoa mipango inayolenga kwa ustawi wa mchango wa michezo kama ala kuu ya kuwasiliana kati ya vijana wa bara moja na kupambana na changamoto zinazokabili michezo ya kiafrika.

 

Na mkutano mnamo kauli za Mawaziri waheshemiwa ulisisitiza juu ya kuimarisha na kusaidia programu kadhaa za mbadilishano kati ya vijana na matukio yanayochangia kuwasiliana kati ya wana wa bara la kiafrika, na kusisitiza juu ya umuhimu wa michezo kama ala kuu ili kuwasiliana kati ya vijana wa bara moja na

kuwaunganisha pamoja na hayo kupitia michezo tofauti si Soka tu.

 

Na Sobhy aliendelea kwa Misri imeweza kutekleza matukio ya michuano na kuitoa kwa njia inayofaa Misri na kwa kiwango cha michezo ya kiafrika iliyokuwa ikishindana na michezo ya kimataifa ili kupeleka ujumbe kwa ulimwengu kwamba Misri inaweza lakini Misri ni moja toka nchi za bara la kiafrika kwa hiyo "Afrika linaweza".

 

Kwa maendeleo, Sobhy alifafanua kwamba wakati wa tangazo la Rais Mheshemiwa kwamba Aswan ni Mji mkuu wa Vijana waafrika 2019, Wizara ya vijana na michezo ilitoa zaidi ya programu 30 mnamo mwaka mzima ili kuhakikisha mikusanyiko kadhaa kwa vijana wa Afrika, kukikamilisha mkakati wa Uongozi wa kisiasa wa kimisri ili kuhakikisha mbadilishano wa kiutamaduni, kisiasa, na kiustarabu kwa nchi za bara la Afrika, na kubadilisha uzoefu kati ya vijana waafrika katika nyanja tofauti.

Comments