"Misri inajadiliana pamoja na taasisi za kimataifa kwa ajili ya kuunga mkono uteklezaji wa Miundombinu barani Afrika. "

 mnamo kipindi kijacho serikali ya kimisri itajadiliana pamoja na taasisi kadhaa za kimataifa kwa ajili ya; kuunga mkono uteklezaji wa miradi ya Miundombinu barani Afrika, pamoja na sekta za Teknolojia ya taarifa, mawasiliano, na nishati endelevu, na kuhimiza sekta binafsi ili kushirikiana, na hayo yote kulingana na Urais wa Misri kwa Umoja wa kiafrika.

 

Na Dokta "Sahar Nasr" "Waziri wa Uwekezaji na Ushirikiano wa kimataifa" amesema kwamba mnamo tarehe ya 7 mwezi wa 5 siku ya jumanne, alikutana na bwana "Benifin Mmika" " Mwakilishi wa Umoja wa ulaya kwa Ushirikiano wa kimataifa na maendeleo ", walitafutiana Ushirikiano mwenye pande tatu, kati ya Misri, Umoja wa ulaya,  na Afrika, kwa lengo la kuunga mkono sekta za Ushirikiano wa kiuchumi na kimaendeleo barani Afrika, na hayo yote kulingana na Urais wa rais "Abd Elfatah Elsisi" kwa Umoja wa kiafrika.

 

 

"Nasr"alieleza kwamba Ushirikiano unakusanya kusaidia mipango ya Ukamilifu wa kikanda kati ya nchi za kiafrika kwenye nyanja za kuhakikisha maendeleo, na Kuangalia kundi jipya la miradi ya maendeleo, kuigharamia, na kuitekleza pamoja na idadi ya taasisi za kimataifa za fedha. Kipindi kijacho Umoja wa ulaya unatafutia ongezeko la Ushirikiano wa maendeleo pamoja na Misri, kupitia mfumo wa uunguaji mkono wa pamoja kati ya Benki na Misri  kwa mwaka wa 2020, katika nyanja za Nishati, Mawasiliano, Majimachafu, Elimu, Afya, na kumwezesha mwanamke, na gharama yake inakaribia kati ya Euro Milioni 432 na 528, ambapo mwakilishi mzungu wa Ushirikiano wa kimataifa na maendeleo amesisitiza kwamba Misri ni nchi muhimu kwa Umoja kwenye eneo la Mashariki ya kati na Afrika, akiongezeka kwamba " Rais Elsisi anaiongoza Misri kwa kutimia mchango mkuu kwenye eneo, kwa kuizingatiwa nguzo kuu ya  Usalama na Utulivu",  akisifu hatua zilizochukuliwa kwa Misri mnamo miaka iliyopita, khasa marekebisho ya kiuchumi yenye nguvu, yaliyochangia kuboresha hali ya Uwekezaji.

Comments