Mnara wa kairo ulijengwa kati ya mwaka 1956 na 1961 ya
saruji kraftigare juu ya jengo la
yungiyungi la kimisri, ambalo liko katikati ya Kairo kwenye kisiwa cha Zamalek
, juu ya kando ya Nile. Ni kimoja cha
vivutio maarufu vya utalii huko Kairo.
Urefu wake ni mita 187 ,Ni mita 43 zaidi kuliko Piramidi Kuu
huko Giza. Juu ya mnara wa kairo kuna mgahawa wa utalii kwenye jukwaa
linalozungukwa na wageni ili kuona mandhari ya kairo kutoka pande zote.
Historia :
Wakati wa ujenzi :
mnara wa Kairo ulijengwa
kati ya 1956 na 1961 na uliyoundwa na mbunifu mmisri Naum Shabib. Washiriki wa
ujenzi huo ni wafanyakazi wamisri mia tano, Maua ya lotus huchukuliwa kama
asili ya pharaoni. Gharama ya kujenga ilikuwa milioni sita za paundi ya kimisri ( 6.000.000 EGP )kwa wakati huo, kiasi
kilicholipwa kwa Marekani kununua nafasi ya Misri bila kitu, na Wamarekani
wanaita jina la mnara "mwiba wa Abdel Nasser," mfano wa ugumu wa
nafasi ya Misri wakati huu.
Kwa mujibu wa riwaya ya mwanahistoria wa marehemu Jamal
Hamdan: Mnara wa Kairo unawakilisha
kauli ndefu mnamo historia “ hapana “, ambapo aliamuru Rais marehemu Gamal
Abdel Nasser kuijenga ujenzi wa kihistoria
"kusema: “hapana” kwa
shinikizo la Marekani juu ya Misri kuacha suala la Algeria, ambako Marekani
ilijaribu kununua sehemu ya Misri kwa fedha kupitia mabalozi wake huko Misri
kupitia mmoja wa wateja wake, lakini uamuzi wa Abdel Nasser ulikuwa kuzitumia
fedha hizi kujenga majengo ya kihistoria. "
Mnara huo umerekebishwa katika mwaka 2006 kwa gharama ya
milioni 15 IE, Na umezidiwa kwa taa jipya la nje kwa kutumia teknolojia mpya ya
taa ili kutoa nishati kwa kiwango kikubwa na inaweza kudhibiti rangi ya mwanga
wa nje wa mnara.
Sifa za Manra :
Mnara wa Kairo una matabaka 16 na ni msingi wa mawe ya Itale
ya Aswan yaliyotumiwa na Wamisri wa kale katika ujenzi wa mahekalu na makaburi
, Katika picha ambayo ni mchanganyiko wa uvumbuaji na kisasa, Mgeni anaweza
kufikia juu ya mnara kupitia Lifti ya umeme katika dakika moja, Mnara huo
unaangalia mji wa Kairo katika mandhari
nzuri sana .
Comments