Katibu wa Shirika la Miji na Serikali za kiafrika: Misri ni uti wa mgongo wa bara

Katibu Mkuu wa Shirika la Miji ya kiafrika na Serikali za kiafrika “ Jean-Pierre Massey ” alisema kuwa shirika linafanya kazi kupitia mtandao ndani ya miji ya kiafrika na mji muhimu zaidi ni Kairo, Johannesburg, mji mkuu wa kiuchumi wa Afrika Kusini, na Lagos, mji mkuu wa kiuchumi wa Nigeria, akiongeza kuwa Misri ni  uti wa mgongo wa  bara la Afrika

Aliongeza kuwa maendeleo ya nchi  huanza kwa kuendeleza maeneo ya ndani na kuiboresha kwa  mitaa katika miji midogo, akisisitiza kwamba maendeleo kwa ujumla yanaunganisha na maendeleo ya maeneo ya ndani, na aliashiria  kuwa baada ya Misri kutawala urais wa Umoja wa Afrika tutakuwa na kitu kipya na mitazamo katika maendeleo ya bara.

 

Kwa upande wa  mahusiano ya kimisri na kiafrika, katibu mkuu wa Shirikisho la Miji ya kiafrika na Serikali za kiafrika alisisitiza kuwa kipindi kilichopita kilikuwa na migogoro mingi, lakini leo Rais Abdel Fattah al-Sisi aliweza kurudisha Misri kwa moyo wa bara la Afrika,na  akisisitiza kwamba Waafrika wanaona Misri kama nguvu kubwa ndani ya bara.

 

Jean-Pierre Massey amekuwa Katibu Mkuu wa Shirika la Miji ya kiafrika na Serikali za kiafrika tangu mwaka 2007,ambapo Shirika hilo lilianzishwa mwaka 2005 na lengo lake la msingi  na  la kwanza ni  kushirikiana kati ya  serikali katika nchi zote za kiafrika ili kuendeleza na kukuza maeneo ya ndani.

Comments