Kocha wa NIGERIA alisema hapingi mfumo wa teknolojia ya mwamuzi msaidizi wa VAR AFCON 2019

KOCHA wa Nigeria, Gernot Rohr ameibuka na kusema kuwa hapingi mfumo wa teknolojia ya mwamuzi msaidizi wa video (VAR) baada ya timu yake kushinda mabao 2-1 dhidi ya Afrika Kuisni juzi katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2019).

Mfumo wa VAR, ambao umeanza kutumika katika hatua ya robo fainali ya Afcon 2019 na umetumika kwa mara ya kwanza katika mashindano hayo, umeingilia maamuzi ya mshika kibendera, Bongani Zungu ukidai kuwa mfungaji aliotea.

 “Ilibidi tusubiri kwa dakika tano, kujua goli au sio goli, na jambo hilo lilikuwa gumu kwa tuimu yangu,” alisema Kocha alipozungumza na waandishi wa habari. “Bao la pili halikuingia na uliona ule mpira wa adhabu, na uamuzi huu wa VAR una walakini kwani huwezi kujua nini kitatokea katika mpira wa adhabu”.

Rohr pia alikipongeza kikosi chake kwa kutoka nyuma kwa 2-1 na kuibuka na kuifunga Cameroon kwa mabao 3-2 katika raundi iliyopita na kupata ushindi wa dakika za mwisho katika mchezo huo wa Jumatano. “Sasa tumeimarika kimawazo na tunaweza kurejea,” alisema. “Tabia ya wachezaji wangu ni ya ajabu...kama kuwa na uhusiano na kila mmoja.”

 Rohr alikumbuka wakati Nigeria ilipofungwa 2-0 na Afrika Kusini nyumbani wakati wa mechi za kufuzu kwa fainali hizo miaka miwili iliyopita, ukiwa mchezo wake wa kwanza akiifundisha timu hiyo.

aliongeza :“Tulikuwa na timu changa lakini timu hii inaendelea kufanya kazi na matokeo haya labda yametusaidia kuifunga Cameroon katika mchezo uliofuata, ambao walikuwa mabingwa wa Afrika, 4-0 kwenye uwanja huo huo (katika mechi ya kufuzu kwa Kombe la dunia, hivyo tumejifunza kutoka katika mechi hii" .

Comments