"Howari Bumedin" Mtu Mwasi Mjenzi Uandaji na Ufasiri " Taasisi ya Tafiti za Ofisi ya Vijana wa kiafrika "
- 2019-07-16 13:02:05
" Muhamed Ebrahim Bukhroba", anayejulikana kwa
Jina la " Howari Bumedin", alizaliwa mashambani mwa Algeria, tarehe
ya 23, mwezi wa 8, mwaka wa 1932, kutokana na familia ndogo na yenye hali dogo
toka Jamii ya wakulima, alikua katika maisha ya kidini, alihifadhi Quraani, na
alisoma Lugha ya Kiarabu, naye ni kama wenzake nchini, alilazimishwa kujiunga
jeshi la Kifaransa, lakini yeye alinuia kukimbia toka Algeria kuelekea Tunisia,
na baada ya Utulivu wa maisha yake nchini Misri, alijiunga kwa Azhar yenye
utukufu, lakini, mnamo zama za mfalme Farouk tawala za kifaransa zilimfuatia
baada ya kukimbia kwake toka huduma ya kijeshi, nazo zilituma barua kwa Ubalozi
wa kifaransa nchini Misri ili kumfukuza toka Misri, isipokuwa mapinduzi adhimu
ya Juli, kwa uongozi wa wanajeshi huru yamemnusuru na yamembakisha nchini
Misri.
Na baada ya Mapinduzi ya Juli, mwaka wa 1973 nchini Misri,
hali ya kisiasa ilikuwa Ipo sawa ili kusanya Elimu na mapambano ya kisiasa,
ambapo ilijihusisha katika chama cha nchi ya Algeria - chenye mapambano makubwa
dhidi ya Ukoloni - nacho kilikuwa kimoja cha wanachama maarufu katika ofisi ya
Morocco ya kiarabu katika Kairo- nacho kilichoundwa na harakati ya kitaifa
katika nchi za Morocco kiarabu( Morocco, Algeria, Tunisia) ; ili kuunganisha
juhudi kwa ajili ya kukomboa Kaskazini ya Afrika kutokana na Ukoloni wa
kifaransa.
Na Misri katika kipindi hicho ilikuwa ikikumbatia harakati
za Ukombozi wa kiarabu na kiafrika, pia ilikuwa Mahali pa Viongozi wa mapambano
dhidi ya Ukoloni, Pamoja na Bumedin, aliyekuwa kiongozi wa harakati za
mashambani ni bwana "Muhamed Bin Abd Elkerim Al Khatabi", kiongozi wa
Kimorocco na mmoja wa mashujaa wa mapambano dhidi ya wafaransa, nayo ilikuwa
mahali pa kuwepo kwake kwa mipango toka ofisi ya Kimorocco ya kiarabu, na chuo
kikuu cha nchi za kiarabu, na rais Abd Elnaser aliamuru kwa kutoa Vifaa na
misaada yote ya kijeshi kwa wenye Mapinduzi wa Algeria hadi Uhuru wake.
Naye alijiunga kwa jeshi la Ukombozi wa kitaifa wa Algeria -
kifungu cha kijeshi cha mwanzo wa Ukombozi wa kitaifa -, katika eneo la
Kimagharibi mwaka wa 1954, na alipambana pamoja na Ahmed Bin Plu hadi Algeria
imepata Uhuru wake, na maisha yake ya kijeshi na cheo chake ziliendelea hadi
alikuwa waziri wa Ulinzi ndani ya serikali ya Bin Plu " serikali ya Uhuru
" mwaka wa 1962,na Bumedin alikuwa akikagua kazi ya Bin Plu vizuri sana,
na ingawa wao walikuwa Marafiki katika safari ya Ukombozi, Lakini Bumedin
hakuwa na Kinaya kwa mtindo wa utawala wa Bin Plu nchini, na kwa hivyo aliamua
kutawala nchi kupitia mabadiliko ya kijeshi dhidi ya Bin Plu mwaka wa 1965, na
bwana Howari alitawala cheo cha rais wa jamhuri, lilijulishwa kwa Mapinduzi ya
Kiraka, mpaka kifo chake mwaka wa 1978.
Bumedin hakuwa na mhusika kama wa Bin Plu, lakini kupitia
Ubora, mafanikio, na kujiamini kwake yeye aliweza kupatia Umaarufu mkubwa sana
toka wananchi. Wakati wa uongozi wake wa Urais, aliweka mipango ya kuendelea
Algeria, na alisisitiza Programu zake, na mwanzoni alitumia Marejeo ya kuuza
mafuta nje vizuri sana, na aliandaa serikali ya " teknokrati"
iliyofanya kazi ya Maendeleo ya kutengeneza mafuta ya kitaifa, na alianza
kutofautiana Programu ya kiwanda, ambapo alihusisha karibu ya nusu ya Uwekezaji
wa kimaendeleo ( unaokadiria kwa milioni dola tano) , kwa upande wa
utengenezaji mnamo kipindi cha( 1970 hadi 1973), na hayo yote yaliwahimiza
wananchi wa Algeria kushirikiana ili kubadilisha nchi yao kwa nchi yenye nguvu
zaidi kuliko zote za nchi za dunia ya tatu. Naye aliangalia Rasilimali ya
kilimo kupitia usawa wa kugawisha vyombo vya kilimo, pamoja na kukuza maisha ya
wakulima, na aliangalia uwanja wa Utamaduni ; kwa ajili ya kurejesha vyanzo
vikuu vya mhusika wa kitaifa wa Algeria, vilivyofichwa kwa ukoloni kama Lugha
na Dini, wakati ambapo alizingatia kugeuka sekta za ( Uongozi, Vyombo Vya
Habari, na Elimu) kwa Lugha ya Kiarabu, lakini lengo hilo halikuhakikisha kwa
Ukamilifu bali ilibakia kwa sura tu.
Na kwa kiwango cha kikanda na kimataifa, Bumedin alikuwa na
mchango mkubwa sana katika kusaidia masuala ya Ukombozi wa kitaifa, na kukuza
suala la kipalestina, basi yeye aliyesema" Algeria Ipo pamoja na Palastena
sawa ikiwa kudhulumu au kudhulumiwa", pia mnamo zama za Bumedin Algeria ilikuwa
nchi ya pili iliyosaidia Misri mnamo vita vya Oktoba 1973, naye alikuwa rais wa
kwanza toka nchi za dunia ya tatu anayezungumza katika Umoja wa kimataifa kwa
Lugha ya Kiarabu, kuhusu Umuhimu wa kuwepo Mpango mpya wa kiuchumi wa
kimataifa, unaoweka mipaka ya Utumiaji wa nchi kubwa dhidi ya nchi dhaifu, pia
aliongoza cheo cha katibu mkuu wa harakati ya kutopendelea ( toka 1973 hadi
1976).
Aliaga dunia tarehe ya 27, mwezi wa 12, mwaka wa 1978,
akiachiwa kurasa nyingi za historia adhimu sana, basi yeye alikuwa Mpiganaji,
mwarabu, mwaminifu, mwafrika, na mwenye fahari, naye aliyesema kwamba"
historia ya nchi ni kama mfululizo wa vita tofauti, hutoka mshindi toka moja
ili kuingia vyenye silaha nyingi kwa vipya, basi tukitoka kutokana na vita vya
Uhuru hii ni silaha ya kuingia vipya, navyo ni vita vya maendeleo, ustawi, na
Maisha
Comments