Wizara ya Michezo inaandaa ziara ya kiutalii kwa Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa kwa Makumbusho ya kimisri
- 2019-07-19 14:18:26
Wizara ya Vijana na Michezo, inayowakilishwa na idara ya Utalii wa
kimichezo kwa ushirikiano na Wizara ya mambo ya kale, ilifanya ziara ya
kiutalii kwa Gianni Infantino rais wa Shirikisho la soka la Kimataifa kwenye
Makumbusho ya kimisri kwa upande wa uwepo wake huko Misri ili kuhudhuria
fainali ya Kombe la mataifa kiafrika siku ya Ijumaa.
Wakati wa matembezi hayo , aliangalia ukumbi wa maonyesho mbalimbali ya
makumbusho na akaanza kutembelea maonyesho ya muda "Spoti kupitia zamani
", ambayo ilifunguliwa na Dokta. Khaled Al Anani, Waziri wa mambo ya kale,
mwezi Juni kwa wakati wa kusherehekea
kwa misri ni mwenyeji ya Kombe la Mataifa ya kiafrika 2019 .
Ambapo maonyesho hujumuisha
vipande 96 vya matoleo yanayoonyesha michezo ambayo vimevutia Wamisri wa kale kuhifadhisha afya ya kimwili, na wamekuwa na nia ya
kuwafundisha watoto wao kufanya zoezi tangu utoto.
Rais wa FIFA pia alitembelea chumba cha Maiti za kale zilizohifadhiwa za
kiufalme (Royal Mummies ) , Mkusanyiko wa Yuya na Toya , chumba cha Tanis , na
chumba cha Mkusanyiko wa Mfalme wa Tutankhamun
Alivutiwa sana na makumbusho na
mabaki yake ya kipekee na ya kale, hasa Barakoa ya dhahabu ya Mfalme
Tutankhamun, sanamu ya Sheikh Al Balad, sanamu ya mfalme Amenhotep III, Mke
wake Ti, na sanamu ya Mfalme Khafra.
pia Rais wa FIFA alivutiwa na njia ya watu wenye mahitaji maalum
mahitaji kutoka vipofu na jinsi wanavyojua kuhusu vipande vya vitu vya
kale kwa njia ya Braille, ambayo
ilifunguliwa na Waziri wa mambo ya kale katika makumbusho kwa ushirikiano na
upande wa Italia , Juni.
Njia hii inajumuisha mabaki 12 ya umri tofauti wa ustaarabu wa kimisri,
kuanzia mwanzo wa zama ya familia, basi nchi ya kale, nchi ya katikati, zama ya
kisasa, wakati wa mwisho na zama za Kigiriki na Kirumi. pia Vipande vilivyochaguliwa
vilijengwa na mawe ya kimisri ngumu kama matale ,pofu anaweza katika njia kutambua kipande kupitia kadi ili kutambua
kitu cha kale kwa lugha ya Braille na vifaa vya sauti vya kielektroniki.
Infantino aliandika katika kitabu
cha ziara cha makumbusho, alielezea ziara yake kwenye ukumbi wa makumbusho kama
nzuri sana na ya kushangaza. Makumbusho inaonyesha vitu vinavyoonyesha
historia, ustaarabu na utamaduni wa utu wote.
Alihitimisha kwa kusema: "Historia ya kushangaza na siku za usoni
(mustakabali ) mkubwa kwa Misri."
Comments