Wizara ya Michezo inaandaa ziara ya kiutalii kwa Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa kwa Makumbusho ya kimisri
- 2019-07-19 14:59:11
Wizara ya
Michezo inaandaa ziara ya kiutalii kwa Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa
kwa Makumbusho ya kimisri
Wizara ya
Vijana na Michezo, inayowakilishwa na idara ya Utalii wa kimichezo kwa
ushirikiano na Wizara ya mambo ya kale, ilifanya ziara ya kiutalii kwa Gianni
Infantino rais wa Shirikisho la soka la Kimataifa kwenye Makumbusho ya kimisri
kwa upande wa uwepo wake huko Misri ili kuhudhuria fainali ya Kombe la mataifa
kiafrika siku ya Ijumaa.
Wakati wa
matembezi hayo , aliangalia ukumbi wa maonyesho mbalimbali ya makumbusho na
akaanza kutembelea maonyesho ya muda "Spoti kupitia zamani ", ambayo
ilifunguliwa na Dokta. Khaled Al Anani, Waziri wa mambo ya kale, mwezi Juni kwa
wakati wa kusherehekea kwa misri ni mwenyeji
ya Kombe la Mataifa ya kiafrika 2019 .
Ambapo maonyesho hujumuisha vipande 96 vya
matoleo yanayoonyesha michezo ambayo vimevutia
Wamisri wa kale kuhifadhisha afya
ya kimwili, na wamekuwa na nia ya kuwafundisha watoto wao kufanya zoezi tangu
utoto.
Rais wa FIFA
pia alitembelea chumba cha Maiti za kale zilizohifadhiwa za kiufalme (Royal
Mummies ) , Mkusanyiko wa Yuya na Toya , chumba cha Tanis , na chumba cha
Mkusanyiko wa Mfalme wa Tutankhamun
Alivutiwa
sana na makumbusho na mabaki yake ya
kipekee na ya kale, hasa Barakoa ya dhahabu ya Mfalme Tutankhamun, sanamu ya
Sheikh Al Balad, sanamu ya mfalme Amenhotep III, Mke wake Ti, na sanamu ya
Mfalme Khafra.
pia Rais wa
FIFA alivutiwa na njia ya watu wenye mahitaji maalum mahitaji kutoka vipofu na
jinsi wanavyojua kuhusu vipande vya vitu vya kale kwa njia ya Braille, ambayo ilifunguliwa na
Waziri wa mambo ya kale katika makumbusho kwa ushirikiano na upande wa Italia ,
Juni.
Njia hii
inajumuisha mabaki 12 ya umri tofauti wa ustaarabu wa kimisri, kuanzia mwanzo
wa zama ya familia, basi nchi ya kale, nchi ya katikati, zama ya kisasa, wakati
wa mwisho na zama za Kigiriki na Kirumi. pia Vipande vilivyochaguliwa
vilijengwa na mawe ya kimisri ngumu kama matale ,pofu anaweza katika njia kutambua kipande kupitia kadi ili kutambua
kitu cha kale kwa lugha ya Braille na vifaa vya sauti vya kielektroniki.
Infantino aliandika katika kitabu cha ziara
cha makumbusho, alielezea ziara yake kwenye ukumbi wa makumbusho kama nzuri
sana na ya kushangaza. Makumbusho inaonyesha vitu vinavyoonyesha historia,
ustaarabu na utamaduni wa utu wote.
Alihitimisha
kwa kusema: "Historia ya kushangaza na siku za usoni (mustakabali ) mkubwa
kwa Misri."
Comments