Algeria imeshinda kwa kombe la mataifa ya Afrika kwa mara ya pili katika historia yake .

Algeria imeshinda kwa kombe la mataifa ya Afrika kwa mara ya pili katika historia yake, baada ya kujipatia goli la mapema dhidi ya Senegal katika fainali iliyochezwa mjini cairo


Algeria yailaza Senegal kushinda kombe la mataifa ya Afrika Afkon 2019 

Shambulio la Baghdad Bounedjah lilimgonga mchezaji wa Senegal Salif Sane na kupita juu ya golikipa Alfred Gomis

Senegal, ambao hajawahi kushinda michuano hiyo , ilipewa penalti baada ya mchezaji wa Algeria kuunawa mpira katika kipindi cha pili lakini refa wa video VAR alibadilisha uamuzi huo na kusema penalti haikufaa kutolewa.

Algeria ilitumia kila mbinu kuwazuia wachezaji wa Senegal waliofanya mashambulizi ya kila aina ili kushinda kombe hilo tangu 1990.

Senegal ambao ilikuwa kushiriki kwa mara ya pili katika fainali tangu 2002 , ilitawala juhudi katika mechi lakini ikashindwa kuzalisha matunda

Comments