Wizara ya Vijana na Michezo inafunga pazia la "ubunifu wa Oskar ya kiafrika"

Wizara ya Vijana na Michezo, inayoongozwa na Dokta. Ashraf Sobhy, ilitangaza utoaji wa Uumbaji wa Oskar wa Kiafrika, iliyoandaliwa na Wizara kupitia idara Kati wa Programu za kiutamaduni na kijitolea , pamoja na ushirikiano wa vijanawenye  ubunifu kutoka nchi za kiafrika, kulingana na  urais wa Misri kwa Umoja wa Afrika. Na katika mfumo wa Aswan, mji mkuu wa vijana wa kiafrika, katika kipindi cha1 hadi 10 Septemba 2019.

Oskar ya ubunifu wa kiafrika inalenga Kuwekeza nguvu na ubunifu wa vijana Waafrika  kutoka nchi  wanachama mbalimbali za  Umoja wa Afrika, Kuonyesha na kuhamasisha vipaji vijana katika nyanja mbalimbali na kuimarisha mahusiano kati ya nchi za Kiafrika kupitia  vijana na sanaa kama njia  haraka zaidi ya mawasiliano na ushirikiano kati ya watu.

Oskar inalenga kuimarisha roho ya ushindani kati ya vijana waafrika  katika nyanja mbalimbali za ubunifu na kuamsha shughuli za kisanii na kiutamaduni za vijana wa nchi za kiafrika.

Vijana waafrika wanashindana wakati wa Oskar katika Nyanja za filamu fupi, uhuishaji, muziki na kuimba, muziki wa mtu binafsi, , kupiga picha, uchoraji, masihara na sanaa pamoja na shughuli za kiufundi . Kamati za uamuzi za Oskar zinajumisha makundi ya wataalam, profesa na wataalamu katika Nyanja zilizopita.

Comments