Katika zama ya Abdelnaser Misri ilikuwa na duru muhimi
katika kuzisaidia harakati za uhuru katika nchi zote za kiafrika na ilitumia
katika usaidizi huo vyombo mbalimbali vya kijeshi, kihabari na kidiplomasia.
Na hata katika wakati ngumu wa Bara la kiafrika kwa sababu
ya ukoloni wa kifaransa na kiingereza, diplomasia ya kimisri haiachi kuzisaidia
ndugu zake (Nchi za kiafrika) ljapokuwa ugomvi wa Abdelnaser na siasa zake
dhidi ya nchi hizi za ukoloni zilizowazuia wadiplomasia wa wamisri kuingia
baadhi ya ardhi za nchi za kiafrika, lakini wadiplomasia wa wamisri ili
wasiache usaidizi wa nchi za kiafrika kwa amri na maelekezo ya Abdelnaser na
hata wanaweza kuwasaidia raia wa nchi hizi katika kupata uhuru wao, walikuwa
wakitumia paspoti ya kilibanon ili waweza kuingia nchi hizi ambapo walikuwa
hawawezi kamwe kuingia nchi hizi kama Msumbiji kwa paspoti ya kimisri.
Comments