Mji huu uko
kando ya Delta ya Nile kaskazini mwa Misri takriban 225 km kutoka Kairo, eneo
lake 100 kilomita mraba .Idadi ya wakazi wake 3,050,000. ni mji mkubwa wa pili nchini Misri na
Afrika. pia ni bandari kubwa katika Misri . ulijengwa mwaka
332 kabla ya kuzaliwa Kristo na Alexander Mkuu, mfalme wa Makedonia kwa
sababu kigriki wameivamia Misri.
Ilikuwa ni kituo cha kisiasa,
kiuchumi, kitamaduni, na biashara. hali ya hewa yake ni kupendeza ,ni
mapumziko ya majira ya joto, unaojulikana kama "bibi
Mediterranean."
Jina la mji limetokana na mfalme Aleksander Mkuu wa Makedonia ya Kale aliyeunda mji huo mwaka 332 kabla ya kuzaliwa kristo .
Waptolemaio waliotawala Misri baada ya Aleksander waliufanya kuwa mji mkuu wa milki yao na kitovu cha elimu na sayansi. Maktaba ya Alexsandria yalikuwa na vitabu vingi kuliko maktaba zote duniani.
Wataalamu toka pande zote za dunia walifika Aleksandria, mji wa elimu, ili kusoma na kunakili vitabu.
Pharos ya
Alexandria ilikuwa mnara wa taa iliyohesabiwa kati ya maajabu saba ya dunia ya
kale.
Usafiri
ndani ya Alexandria huenda kwa kutumia barabara, njia za reli na reli ya juu ya ardhi "Tram" . Kuna
teksi na mabasi ambayo ni ya umma au ya binafsi. Njia nyingi za
mabasi yanakutana kwenye El-Mawaf .
Alexandria
ilipata umaarufu mkubwa kwa sababu ya wakazi wake kama mwana wa fasihi Tawfik
El Hakim , mtaalamu wa fani ya ujenzi Hassan Fathi , mshairi Kostantin Kafafes
, mwanamuziki Sayed Darwish , msanii Amr El Sherif , bingwa wa kuogolea Abo
Hief na mtengenezaji wa filamu Yossef
Shahin.
Vivutio vya
Alexandria:
Nguzo
ya El- Sawari
Ni miongoni
wa maeneo ya kale yaliyo maarufu zaidi mjini Alexandria . iko juu ya kilima cha
kale Kom El- Shakafa . Urefu wake ni
takriban mita 27 . Ilijengwa mnamo karne ya tatu baada ya kuzaliwa Kristo kama
ni kumbukumbu ya mfalme Diklanyos .
Jukwaa la
kiroma
Lipo
katikati ya Alexandria katika eneo Kom El-deka . lilijengwa mwanzoni mwa karne
ya nne baada ya kuzaliwa Kristo .
Boma la
Qaitbay
Iiko
magharibi mwa Alexandria katika eneo Bahari . lilijengwa kuanzia tarehe 882
hadi 884 baada ya Hijra ya mtume.
Maktaba mpya
ya Alexandria
Ni alama ya
kiutamaduni iliyojulikana ulimwenguni kote . Iko eneo la Shatbi karibu ya
bahari la Mediterranean . Inajumuisha vitabu
ambavyo idadi zao ni zaidi ya milioni 8 .
Comments