Waziri wa vijana na michezo anapongeza timu ya taifa ya Misri ya mpira wa mikono baada ya kufikia kwake robo fainali katika michuano ya dunia.

 Waziri wa vijana na michezo, Dokta Ashraf Sobhy amewapongeza wachezaji wa timu ya taifa ya Misri ya mpira wa mikono na baraza la uongozi wa Muungano baada ya kufikia kwake robo fainali katika michuano ya dunia inayofanyika sasa nchini Uhispania.

 

Sobhy amesifu  juhudi za kipekee ambazo wachezaji wanazitoa, ambapo wachezaji wameweza kufuzu katika sekunde za mwisho ili timu ya taifa ya Misri inashinda dhidi ya timu ya taifa ya Serbia kwa tija 30/29, na kufikia robo fainali.

 

Sobhy amesisitizia imani yake katika wachezaji, akitamani ushindi wao kwa michuano hiyo, akiashiria kufuata kwake kwa tija yenye heshima iliyohakikishwa mpaka sasa.

 

Inabidi kutaja kuwa wizara ya vijana na michezo inajitahidi sana katika kusaidia wachezaji na kutoa msaada wa kila aina kwao ili kushinda michuano nyingi na kuheshimu nchi ya Misri katika michuano ya kimataifa

Comments