Vijana wa timu ya kitaifa ya Misri ya mpira wa mikono wanashinda timu ya kitaifa ya Norway kwa matokeo 29/27 na kufikia mraba wa kidhahabu (nusu ya fainali) katika kombe la dunia .

Timu ya kitaifa ya Misri ya mpira wa mikono ya vijana imeweza kufuzu dhidi ya mwenzake, timu ya taifa ya Norway kwa matokeo 29/27 katika robo fainali ya kombe la dunia linalofanyika nchini Uhispania, ili kufikia mraba wa kidhahabu (nusu ya fainali).

 

Kipindi cha kwanza kimeisha kwa ucheleweshaji wa timu ya taifa ya Misri kwa Matokeo  12/14, licha ya kimweko cha kipekee kwa wachezaji wawili wa timu ya kitaifa ya Misri ya vijana, (Mohsen Ramadan) ambaye ni mfungaji bora wa magoli katika mechi iliyopita dhidi ya timu ya kitaifa ya Serbia na mwenzake (Seif Alderaa), lakini wakati wa kipindi cha pili imeonekana nguvu kutoka upande wa Norway, hususan wachezaji wa (wing), kabla ya timu ya taifa ya Misri inaweza kurudi kwa mechi ili kupunguza tofauti ya magoli na kufunga magoli mengi zaidi.

 

Timu ya taifa ya Norway ya mpira wa mikono ya vijana imefikia robo ya fainali baada ya kufuzu dhidi ya timu ya kitaifa ya Brazil katika raundi ya 16, huku timu yetu ya taifa ya Misri imefikia robo fainali baada ya kufuzu dhidi ya timu ya taifa ya Serbia kwa matokeo 30/29.

Na mechi za timu ya taifa ya Misri ya mpira wa mikono ya vijana katika zamu ya kwanza kwa kombe la dunia zimeshuhudia ushindi wa timu ya taifa ya Misri dhidi ya timu ya taifa ya Australia katika ufunguzi wa mechi zake kwa kombe la dunia,siku ya Jumanne kwa matokeo  44/17, baadaye imeshindwa timu ya taifa ya Nigeria katika mechi yake ya pili ya siku ya Jumatano kwa matokeo 47/30, kisha imepata mapumziko kutoka mechi siku ya Alhamisi, kisha imeshindwa timu ya taifa ya Uswidi kwa matokeo  32/22, pia imehakikisha ushindi wa stahiki dhidi ya timu ya taifa ya Korea Kusini kwa matokeo 38/36 katika siku ya Jumamosi, na hatimaye imehakikisha mshangao wa ushindi dhidi ya timu ya kitaifa ya Ufaransa kwa matokeo  37/32.

Comments