Waziri wa vijana na michezo, Dokta Ashraf Sobhy anampongeza Farida Osman kwa kufikia fainali ya mashindano ya mita 50 ya kipepeo katika michuano ya dunia nchini Korea Kusini.

Dokta Ashraf Sobhy anampongeza mwoga wa Kimisri Farida Osman baada ya kufikia kwake fainali ya michuano ya dunia kwa kuogelea inayofanyika sasa nchini Korea katika mashindano ya mita 50 ya kipepeo mnamo muda wa  sekunde 25:79 kwa mara ya nne mfululizo.

 

Waziri wa vijana na michezo amesifu ngazi ya kipekee ambayo bingwa wa Kimisri ameitoa katika michuano ya dunia, akisisitiza kuendelea kwake katika kutoa misaada kwa bingwa wa Kimisri kwa ajili ya kuhakikisha medali nyingi zaidi katika michuano hiyo.

 

Sobhy amesifu juhudi zinazofanywa kwa Muugano wa Kimisri ya kuogelea kwa ajili ya  kuhakikisha tija hizo za kuheshimu. 

Comments