masanamu makubwa ya Ramsisi wa pili jijini Abu Sembel, nchini
Misri. Historia yake inarudi miaka 1400 B.C
Uandishaji wa kurasa za mwanzo za daftari la historia
zimeanza takriban tokea miaka ya 3300 K.K. kaskazini mwa Afrika kwa kuchomoza
nyota ya ustaarabu wa kifarao nchini Misri ya kale. inazingatiwa ni moja ya
staarabu kongwe Zaidi zilizobaki. ustaarabu wa Misri ulikuwa na athari katika
maeneo mengi mpaka mwaka 343 K.K. kuathiri kwa ustaarabu wa Misri upande wa
magharibi kumefika hadi Libya ya hivi sasa, na ukafika Kriti na Kanaani kwa
upande wa kaskazini, na ufalme wa Aksomi na Nuba kwa upande wa kusini,
kukaundwa kituo huru kinachonufaika na mahusiano ya kibiashara pamoja na
Wafiniki katika maeneo ya Kartaji kwenye mwambao wa kaskazini magharibi mwa
Afrika.
ugunduzi wa Ulaya barani Afrika umeanza tangu zama za ustaarabu
wa kirumi na wa Kireno wa kale. katika mwaka 332 K.K. Misri imemkaribisha
Skandar Mkubwa Zaidi ikimzingatia kuwa ndio mkombozi wa Misri kutokana na
mavamizi ya kifursi dhidi ya Misri. Akaanzisha mji wa Alexandria nchini
Misri ambao umekuwa ndio mji mkuu ,
ulioimarika na ukoo wa watawala wa Maptolemi baada ya kufa kwake. Baada ya
mavamizi ya utawala wa kibeberu wa kirumi kwa maeneo yaliyorefuka kwenye bahari
ya Kati na kaskazini mwa Afrika, eneo hili
la kiuchumi na kiutamaduni, lilikuwa chini ya utawala wa kirumi.
utawala kali wa kirumi umeishikilia eneo linalojumuisha Tunisia ya leo
na maeneo mengine katika mwambao wote.
Comments