Wizara ya Mawasiliano inaangalia pendekezo la barua la kimataifa kuzindua jukwaa la Biashara ya elektroniki barani Afrika

Wizara ya mawasiliano na teknolojia ya habari  ilisema kwamba ilimpokea "Bashar Hussein," Mkurugenzi Mkuu wa ofisi ya kimataifa ya Jumuia ya barua ya kitaifa , ambapo wakati wa mkutano imebadilishwa maoni kuhusu idadi ya maswala kadhaa yanayohusiana na sera za udhibiti za taasisi za barua ,Na hiyo kwa mahudhurio ya "Essam Saghir" Mwenyekiti wa bodi ya Idara ya mamlaka ya kitaifa ya barua .

 

Na ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Kimataifa ya Jumuia ya barua ya kitaifa kwa Misri inakuja katika mfumo wa kukaribisha mji wa Sharm El Sheikh kwa matukio ya mkutano wa mkakati wa Kikanda kwa  eneo la Kiarabu 2019.

 

Wakati wa mkutano huo, wizara ilisisitiza hamu ya Misri katika ushirikiano wa kimataifa na ushiriki mzuri  katika baraza la kimataifa linalohusika na kuanzisha sera za kisheria za maendeleo ya sekta ya barua, akionyesha umuhimu wa endelea taasisi za barua kwa maendeleo ya kiteknolojia ya ulimwengu ambyo yanalenga kupanua aina za huduma zinazotolewa kwa raia .

 

 

Na wakati wa mkutano huo , wizara ilikagua juhudi zilizofanywa na Misri ili kuongeza faida ya barua ya Misri katika kutekeleza mkakati wa Misiri wa mabadiliko ya kihesabu kwa kuzingatia uwezo wake na kuenea kupitia ofisi za barua 4,000 nchini. Akiashiria kwa maendeleo ambayo zinashuhudia ofisi za barua Kubadilishwa kwa vituo vya kutoa huduma za barua, kifedha na serikali ,Pamoja na kutoa mchango katika kusaidia ujasiriamali kupitia ushirikiano na taasisi ya maendeleo ya mradi ndogo na ya Kati na ndogo sana katika kutoa huduma za utoaji wa fedha miradi ndogo na ndogo sana kwa wateja wa taasisi na uuzaji wa bidhaa za mikono na bidhaa za urithi kwenye tovuti ya Mamlaka ya barua ya Kitaifa.

 

Kwa upande wake,Bashar Hussein alisifu michakato ya maendeleo iliyoshuhudiiwa kwa  Ofisi ya Barua ya Misiri ambayo yanaambatana na sera za Jumuiya ya barua ya ulimwengu , Ili kuamsha jukumu la taasisi za barua katika kufanikisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

 

 Na wakati wa mkutano , Bashar Hussein alipendekeza kuzindua  jukwaa la Biashara ya elektroniki barani Afrika, ambapo Wizara ilikaribisha pendekezo hili, ikisisitiza umuhimu wa kuandaa masomo inahitajika ku tekeleza jukwaa hili.

 

 Ni muhimu kutaja kwamba  Umoja wa barua Ulimwenguni una nchi 192  na ndio jukwaa kuu la ushirikiano kati ya watendaji wenye ufanisi katika sekta ya barua  ulimwenguni, Na unavutiwa na kuweka sheria za kubadilishana barua za kimataifa na kutoa mapendekezo ya kuchochea ukuaji wa saizi ya barua , vifurushi na huduma za kifedha na kuboresha ubora wa huduma ya wateja.

Comments