Piramidi za Giza

Ni kati ya majengo yanayojulikana zaidi duniani zipo kando ya mto wa Nile .Piramidi hizo ni mabaki ya eneo kubwa la makaburi ya enzi za Misri ya kale.Wafalme na maafisa ya juu walizikwa hapo .Wamisri wa zamani waliamini kuwa mfalme alikuwa na nguvu zisizo la kawaida na kuwa amechaguliwa na Mungu kwa kuambatanishi binadamu duniani na kwa sababu hii mfalme alipata heshima kubwa hata alipofariki .Wamisri wa zamani waliamini kuwa sehemu ya roho ya mfalme hubaki na mwili baada ya kifo chake ,ili kuutunza mwili wake wametumia dawa maalumu za kuutunza .Alizikwa na vitu vilivyohitaji kabla ya kifo chake kama dhahabu,chakula,mavazi na fenichia N.K.watafiti wa mambo ya kale wanakadiria kuwa jumla ya wafanyikazi elfu kumi waliotumiwa kwa ajili ya kujenga piramidi hizo .

Nazo ni:

Piramidi kuu ya Giza iliyoko mbali wa kilomita 15 kusini magharibi mwa mji mkuu wa Misri,Kairo .Ilijengwa kama eneo la kaburi la farao Khufu mfalme wa Misri miaka 2551 kabla ya kuzaliwa Kristo .Piramidi hiyo ina urefu wa futi 481 ikiwa ndio kubwa zaidi kuwahi kujengwa na jengo refu zaidi duniani katika karne ya 19 . Piramidi hiyo imewashangaza wengi kwa ukubwa na umaridadi wake na si ya ajabu iliyooradheshwa kati ya maajabu saba ya ulimwengu wa kale . Piramidi hiyo ambayo imedumu kwa zaidi ya miaka 4500 ndio pekee iliyosalia katika maajabu saba ya ulmwengu wa kale . Je, farao Khufu alikuwa nani ? Khufu alikuwa mfalme wa pili katika milki ya nne ya ufalme wa kale wa Misri . Alitawala kwa miaka 23 .Khufu alikuwa mwana wa pekee wa farao Sneferu na malikia Hetepheres wa kwanza . Khufu  ndio farao wa kwanza kujenga piramidi .Inaaminika kuwa alikuwa na wake watatu . Piramidi hii kuu ni kazi ya wahandisi wa hali ya juu inayowashangaza hata wajenzi wa leo, ilizingatiwa kuwa wajenzi wa kale walitumia vifaa vya shaba na shaba nyekundu kwa ujenzi.Maarifa hayo ya kipekee yamewazuzua wengi kwa karne nyingi .Inasemekana kwamba mradi huo ilichukua miaka 30 kukamilika ;miaka 10 ya maandalizi na 20 ya ujenzi .Piramidi hiyo iko mwamba tambarare iliyo katika ukingo wa magharibi ya mto wa Nile kaskazini mwa nchi ya Misri .Wakati wa ujenzi wake hakukwepo majengo mengine eneo hilo ,na baada ya muda fulani piramidi nyingine zilijengwa .Ni jengo kuu kwenye ardhi yenye ukubwa wa ikari 13 . Kila upande ukiwa na urefu wa futi 756 . Jengo hilo limejengwa kwa mawe milioni 2.3 mawe mazito na makubwa zaidi ;kila moja lilikuwa na uzito tani 2.5 . Kubwa zaidi lilikuwa na uzani wa tani 15.

Piramidi ya Khefren

Ni moja ya Piramidi za Misri ya kale. Piramidi hiyo iko mwamba tambarare iliyo katika ukingo wa magharibi ya mto wa Nile kaskazini mwa nchi ya Misri.Inachukua nafasi ya pili katika ukubwa baada ya Piramidi ya farao Khufu .Ilijengwa na mfalme Khefren ambaye ni mfalme wa nne katika milki ya nne ya ufalme wa Misri ya kale .Alitawala Misri kuanzia tarehe 2559:2535 kabla ya kuzaliwa Kristo .Alijenga Piramidi ya Khefren wakati wa ufalme wake.Piramidi hiyo ni jengo kuu kwenye ardhi yenye ukubwa mita miraba 215 na ina milango miwili katika upande wa kaskazini .Piramidi hiyo ipo kusini magharibi mwa piramidi ya babake Khufu. Urefu wake ni mita 143 na sana hivi ina urefu wa mita 136 .kila upande ukiwa na urefu wa mita 215.5 .

Piramidi ya Mykerions

Mfalme Mykerions ni mfalme wa tano katika milki ya nne ya ufalme wa Misri ya kale . Alichukua ufalme baada ya kifo cha babake Khefren. Inasemekana kwamba alitawala Misri kwa muda ya miaka 18.Piramidi hiyo ni miongoni mwa piramidi za Giza nchini Misri.Ilijengwa na mfalme Mykerions lakini haikukamilika katika ufalme wake bali ilikamilika katika ufalme wa mfalme aliyemfuata Shepseskaf na hivyo kwa kutumia matofali ya kuchoma .Piramidi hiyo ina urefu wa mita 65.5 lakini sasa hivi ina urefu wa mita 62 baada ya sura yake ya nje imeboromoka . Kila upande ukiwa na urefu wa mita 108.5 .

Comments