Misri inachukua nafasi ya nne duniani katika mbio ya mfulilizo ya 4×100 katika michuano ya mapezi.

Timu ya kitaifa ya Misri kwa kuogelea kwa Mapezi imeshinda nafasi ya nne duniani katika mbio ya mfulilizo ya

mita 4×100  "wanawake"  ya kuogelea kwa mapezi juu ya maji miongoni mwa mashindano ya michuano ya dunia, baada ya mashindano makali dhidi ya timu za taifa za Urusi, Ukraine na Hungary

Tija hiyo ni bora zaidi kwa timu ya kitaifa ya Misri inayoshiriki katika michuano ya dunia ya kuogelea kwa mapezi inayofanyika mjini Sharm El sheikh mnamo kipindi cha tarehe ya  ishirini na nane, mwezi wa Julai hadi siku ya nne kutoka mwezi wa Agosti.

 

Timu ya kitaifa ya Urusi imeshinda kwa nafasi ya kwanza, Ukraine imeshinda kwa nafasi ya pili, Hungary imeshinda kwa nafasi ya tatu na Misri imekuja katika nafasi ya nne.

Katika wakati huo huo, mwogaji mmisri ( Judy sherif Almas), ambaye ni mchezaji wa klabu ya (Al itihad Alsakandy) amevunja rekodi ya Misri kwa  mbio ya mita 100 ya kuogelea kwa mapezi juu ya maji, ambayo ni 43:72 na imekuwa 41:91.

 

Kwa upande mwingine, mashindano ya awamu ya pili kwa michuano ambayo ni kuogelea katika maji wazi yanaanza leo Jumamosi, baada ya hitimisho ya mashindano ya (Mono, Mapezi ya mbili na mfululizo).

Nchi 14 zinashirikisha katika mashindano ya kuogelea katika maji wazi, ambapo mbio zitafanyika kwa vipindi viwili, kipindi cha Asubuhi kitaanzia mbio ya mfulilizo ya Mita 2×4 na kipindi cha jioni kitaanzia mbio za kilometa 6 za kibinafsi. 

Comments