Sobhy alimheshimu Farida Othman baada ya kushinda medali ya shaba katika Mashindano ya Dunia kwa Kuogelea
- 2019-08-05 16:23:29
Waziri wa
Vijana na Michezo Dokta Ashraf Sobhy alimheshimu mwogaji mmisri Farida Othman baada ya
kushinda medali ya shaba katika mbio ya mita 50 kwa wanawake , Katika
Mashindano ya Dunia ambayo iiyokaribishwa na Korea Kusini wakati wa kipindi cha
2 hadi 28 Julai iliyopita, kwa kuwepo Dokta Hisham Othman baba wa mchezaji,
Yasser Idris, Mwenyekiti wa baraza la Wakurugenzi wa Shirikisho la kimisri kwa
Kuogelea.
Waziri wa
Michezo alisisitiza kwamba medali iliyohakikishwa na bingwa wa Misri ni
mafanikio ya kihistoria kwa Misri pamoja na mafanikio yaliyohakikishwa na timu
ya kitaifa kwa mpira wa mikono baada ya imeshinda kwa medali ya shaba katika
mashindano ya dunia , akibainisha kwamba Wizara ya Michezo inaunga mkono
mashirika yote ya kimichezo ili kutoa misaada kamili kwao na kutoa mahitaji ya
kisaikolojia na kifedha kwa kuhahikisha mafanikio bora zaidi.
Sobhy
alizisifu juhudi na matokeo yaliyohakikishwa na mchezaji Farida Othman. pia
Alizisifu juhudi zilizofanywa kutoka Shirikisho la kimisri kwa Kuogelea katika
kuandaa mchezaji huyo kisaikolojia na kumtibu kutokana na jeraha.Alisifu
kiwango cha kisanii bora ambacho shujaa wa Misri Farida Othman ameonyesha
wakati wa mashindano, na kumtaka aendeleze kufanikiwa na heshima. Misiri katika
vikao vya kimataifa.
Waziri wa
Michezo alisifu kiwango bora cha kiufundi ambacho shujaa mmisri Farida Othman
alionyesha wakati wa mashindano, akiashiria ufuatiliaji wa matokeo unaoendelea
katika kipindi cha mashindano , ametamani kwake kuendelea na mafanikio yake na
heshima ya Misri katika matukio ya kimataifa.
Dokta Ashraf
Sobhy alijadili maandalizi ya hivi karibuni kwa kikao cha Michezo ya Olimpiki
ya Tokyo 2020 na maandalizi ya bingwa Farida Othman kwa ajili ya mashindano,
akitarajia kupata medali ambayo iliwafurahisha watu waamisri, ambao wanangojea
medali zaidi.
Kwa heshima
yake, Waziri wa Michezo aliamua kuandaa siku ya maadhimisho ya mchezaji Farida
Othman katika eneo la beseni ya kuogelea kwenye Kituo cha Vijana cha AL-Jazira,
kilichoanzishwa na Wizara ya Vijana na Michezo kwa kutambua historia yake ,na
sera yake ya kimichezo katika kiwango cha kimataifa.
Comments