Ujumbe wa Jumuia ya Ushirikiano wa Kimataifa ya Japan (JICA) unataka kusambaza Jaribio la Misiri katika kilimo cha mpunga nchini mwa kiafrika.

Dokta Tamer Farouk , Mratibu wa Mpango ya Mafunzo ya kilimo cha mpunga kwa Waafrika , Na Mfadhili na (JICA) wa Japani, alisema kuwa wajumbe wa ujumbe wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kimataifa ya Japan (JICA) katika ofisi ya Misri walifuatilia mpango wa mafunzo katika Kituo cha Utafiti na Mafunzo huko Sakha, Mkoa wa Kafr El-Sheikh.

 

Farouk ameongeza kuwa ujumbe huo umetambua shughuli mbali mbali za utafiti, Na akiashiria kuwa "Yoshifumi Amora," Mkurugenzi wa Ofisi ya(JICA) ya Misri alisifu juhudi za watafiti, Anataka mwendelezo wa ushirikiano kati ya Misiri na Japani kwa maendeleo ya mazao ya mpunga barani Afrika, Hasa na Rais "Abdel Fattah El Sisi" kuchukua urais wa Umoja wa Afrika.

 

Dokta "Mahmoud Abu Yusuf", mkuu wa mpango wa uzalishaji wa mibegu, ameongeza kuwa Wajumbe wa ujumbe huo walisifu uzoefu wa Wamisri katika kukuza mazao ya mpunga, wakisisitiza hitaji la kusambaza uzoefu huu katika nchi mbali mbali za Kiafrika.

Comments