Thoma
aliyependwa na mamilioni ya wananchi katika kipindi cha miaka hamsini ya kazi
bora na mafanikio.Alijulikana kwa sababu ya sauti yake nzuri na historia yake
iliyojaa na changamoto kadhaa.Alipania kuchapa kazi hadi mwisho wa umri
wake.Amewapa wananchi fani nzuri kabisa.Nyimbo zake zimeitaka nyara mioyo ya
waarabu wore mnamo miaka mengi.
Kwa ukweli
ingawa Om Kalthom aliaga dunia miaka 40 iliyopita ila fani yake bado ipo.Nyimbo
zake zipo akilini mwa mamilioni ya wasikilizaji wake hadi leo.Fani yake kama
taa iliyoangaza maisha yetu.
Maisha ya Om
Kalthom kwa ufupi.
Jina lake
halisi no Fatuma Ebrahim El_Sayed El_Biltaji . Alikuwa na majina ya utani
kadhaa kama vile Thoma,Jumuia ya mataifa ya kiarabu,kizeze cha mataifa ya
kiarabu,sayari ya mashiriki ya kati na fanani wa umma.
Om Kalthom
alizingatiwa kuwa ni moja ya waimbaji mashuhuri wa karne 20 . Alianza maisha
yake ya fani utotoni mwake.Alipata umaarufu nchini Misri na nchi za kiarabu.
Alizaliwa
tarehe 31 Disemba mwaka 1898 katika kijiji kidogo karibu ya El_Mansoura
kinachoitwa Tamay El_Zaharia mkoa wa El_Dakahlaya.Hakuna mtu yeyote anaamini
kwamba msichana huyu wa familia masikini aliyeishi katika kijiji bila ya shule
hata moja atakuwa mashuhuri sana.Lakini alipata umaarufu utotoni mwake kiasi
kwamba baba yake alifanya urafiki na sheikh zakaria Ahmed na Sheikh Aboila
Mohamed waliokuja mtaani El_Senbaliwen ili kuandaa sherehe kadhaa mwezi wa
Ramadan Mtukufu.Hawa walimshawishi baba ya Om Kalthom kuhama kairo na binti
yake.Hii ilikuwa hatua ya kwanza katika maisha yake ya kifani.Wakati huu
aliimba katika sherehe ya kuadhamisha kumbukumbu ya El_Esra na El_Marag Katika
jumba la "Azz El_Din Yakin" na malipo yake alikuwa pete ya dhahabu na
paundi tatu kutoka kwa bibi wa jumba.
Mwaka 1921
Om Kalthom alirejea mara tena mjini kairo ili kuimba na timu ya babake.Alipata
fursa ya sauti yake inasikika mjini Kairo na sauti yake ilipata kupendwa na
sheikh Ali Mahmoud, sheikh Ali El_Kasabgi na hasa sheikh Aboellah Mohamed
alikuwa mwalimu wake na alimsihi kuimba katika nyanja nyingine baadala ya
nyimbo za kidini.
Mwaka
1923 Om Kalthom alianza kuimba katika
majumba ya wakuu wa Kairo.Baadaye alianza kupata umaarufu zaidi na alishindana
na mabingwa wa uimbaji wa wakati huu kama Naima El_Masrry,Monira
El_Mahdia,Fatuma Series na Fathia Ahmed.
Mwaka 1924
sheikh Aboellah alimsindikiza Om Kalthom hadi mshairi Ahmed El_Romi aliyechukua
jukumu LA l kumfundisha Om Kalthom lugha na ushairi.
Om Kalthom
alishiriki katika filamu kwa mara ya kwanza mwaka 1936 kwa anwani ya Widad
alikuwa mhusika mkuu na aliimba ndani yake.Baadaye alishiriki Katika filamu
tano nyingine. Filamu ya mwisho ilikuwa Fatuma mwaka 1947.Filamu hizo ni Ayda
mwaka 1942,Nashid El_Amal mwaka 1937,Salama mwaka 1945 na Dananir mwaka 1947.
Om Kalthom
alipata tuzo kadhaa katika maisha yake ya kifani kutoka nchi nyingine kama
Lebanon,Misri,Jardan , Iraq,Moroco,Tunisia,Libya,Sudan na Pakistan.
Tarehe 3
mwezi wa Februari mwaka 1975 Thoma aliaga dunia alikuwa na umri Wa miaka 73 baada
ya miaka kadhaa ya ugonjwa.Wafuasi wake na mataifa ya kiarabu walifanya mazishi
makubwa . Thoma aliacha urithi wa kifani kwa fani ya Misri na ya Kiarabu.
Matembeleo
ya Om Kalthom katika mataifa ya kiarabu barani Afrika
Historia
itaendelea kuwa ithibati ya mafanikio ya bingwa la uimbaji Om Kalthom.
Kwa ukweli
bibi Huyu alikuwa kama mti mwenye matawi mengi . kiasi kwamba aliweza
kuwaunganisha waarabu wote.Alikuwa anaipenda sana Misri.Kiasi kwamba alitumia
Uimbaji kama nguvu laini Kupita uimbaji aliweza kusanya pesa kwa ajili jeshi ya Misri inunue
silaha baada ya vita mwaka 1967.
Mfuatiliaji
wa historia ya Om Kalthom hufahamu kwamba maisha yake yameisaidia Misri kwa
hali na Mali katika vipindi vyote vya kihistoria kwani alikuwa na uzito wa
kisanaa. Maisha yake hakuwa uimbaji tu kwa ukweli alikuwa balozi wa fani ya
kiarabu na ya kiafrika .Alifanya matembeleo kadhaa ya uimbaji katika mataifa ya
kiarabu kama Sudan,Tunisia,Libya na Morocco ili kusanya pesa kwa ajili ya
kuisaidia jeshi ya Misri baada ya vita mwaka 1967.Matembeleo haya ya kihistoria
bado ipo katika kumbukumbu ya kiarabu na ya Kiafrika.
Comments