wakati wa wiki ya Ndugu ya kimisri-kimorocco... Wizara ya Vijana na Michezo inapokea ujumbe wa vijana kutoka Ufalme wa Morocco

Wizara ya Vijana na Michezo imepokea ujumbe wa vijana kutoka Ufalme wa Morocco kushiriki katika shughuli za Wiki ya Ndugu ya Kimisri Kimorocco, ambayo inatekelezwa na Wizara ya Vijana na Michezo kupitia Idara kuu ya Programu za Utamaduni na kujitolea na inaendelea hadi tarehe 25 Agosti 2019 huko Kairo na Aleskandaria .

Taarifa ya Wizara ya Vijana na Michezo ilieleza kwamba ziara hiyo inakuja katika mraba wa  kukuza na kuunganisha uhusiano kati ya nchi hizo mbili kupitia vijana, katika utekelezaji wa mpango wa utendaji na ushirikiano katika uwanja wa vijana kati ya Wizara ya Vijana na Michezo ya Misri na mwenzake wa Morocco.

 

Taarifa hiyo iliashiria kuwa Wizara ya Vijana na Michezo imeandaa mpango wa kiutalii wa kitamaduni kwa wajumbe walioshiriki, ili kufahamiana na tamaduni ya Wamisri na kubadilishana utamaduni kati ya nchi hizo mbili kupitia mazungumzo na kutembelea maeneo ya kiutalii na kihistoria katika Jamhuri ya Kiarabu ya Misri.

 

Taarifa hiyo ilisisitiza kuwa wiki ya Ndugu ya Kimisri-Kimorocco inakuja katika mraba wa mkakati wa Wizara ya Vijana na Michezo ili kuongeza uhusiano kati ya Jamhuri ya Kiarabu ya Misri na Ufalme wa Morocco kupitia vijana, ikizingatia kwamba Misiri na Morocco zina uhusiano wa kihistoria na uhusiano uliotofautishwa katika nyanja zote, na hii inaimarisha kubadilishana kwa vijana kati ya nchi hizo mbili.

 

Taarifa hiyo ilionyesha kuwa mpango wa wiki ya Ndugu  inajumuisha kutembelea Aleskandaria kutambua maeneo ya utalii na ya kiathari , na pia kutembelea piramidi za Giza ili kuona ukuu wa ustaarabu wa Misri.

 

Programu hiyo ya wiki inajumuisha pia matembezi ya majumba ya kumbukumbu ya Wamisri, pamoja na Jumba la Makumbusho ya Kikosi cha Hewa na Jumba la Makumbusho la Misri, Ziara ya Jumuiya ya Dini na ngome ya Salah al-Din , ziara ya Mtaa wa Al-Moez, Khan Al-Khalili na eneo la Al-Hussein, utekelezaji wa matembezi ya uhuru , pamoja na utekelezaji wa maonyesho ya kisanii ya Misri-Moroko katika Kituo cha vijana wa kisiwa na kuandaa kwa maonyesho ya kazi za urithi kuhusu utamaduni wa nchi hizo mbili

Comments